Buhari akiwa na mwenyeji wake Obama alipoitembelea Marekani |
Marekani "inawasaidia na kuchochea " kundi la wanamgambo wa kiislam wa Boko Haram kwa kukataa kutoa silaha kwa Nigeria, ni kauli ya rais wa Nigeria Mahammadu Buhari.
Sheria ya Marekani inazuia serikali kuuza silaha kwa nchi ambazo zinashindwa kushughulikia ipasavyo masuala ya haki za binadamu.
Boko Haramu hutekeleza pia visa vya mauaji na utekaji wa wanawake na watoto |
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alikutana na rais Barack Obama Jumatatu kuomba msaada zaidi.
Boko Haram limewauwa watu 10,000 tangu mwaka 2009 na limewateka mamia ya wasichana na wanawake.
Source: BBC
No comments :
Post a Comment