Saturday, July 18, 2015

KUFUATIA TUHUMA ZA KUGUSHI: MMILIKI WA MABASI YA UDA ASAKWA

Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Robert Kisena
Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Robert Kisena
Dar es salaam: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kumkamata mmiliki wa mabasi ya UDA Robert Kisena pamoja na aliyekua Ofisa ukaguzi mwandamizi wa Benki ya TIB, Adam Yusuph. Hati hizo zilitolewa kutokana na
watuhumiwa kushindwa kuhudhuria mahakamani kwa ajili ya kusikiliza mashitaka yanayowakabili ya  kughushi nyaraka mbalimbali za malipo.


Mwingine anayekabiliwa na shitaka hilo ni pamoja na muhasibu wa Simon Group, Venancy Matondo aliyeunganishwa   wanadaiwa kudhamiria kughushi hati ya malipo kuonyesha kuwa chama cha ushirika cha Shinyanga  kilisambaza  mbegu zenye thamani ya Sh. 145 milioni.
Hakimu Thomas Simba alitoa hati hiyo ya kukamatwa  baada ya mwendesha mashitaka kwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Josheph Kiula kudai kuwa Kisena alifikishiwa wito wa kuitwa mahakamani na akausaini , lakini jana hakutokea  mahakamani na hivyo kuomba hati ya kumkamata."
Kiula  alidaiwa kuwa, walimpigia simu mkurugenzi huyo mtendaji  wa kampuni ya Simon Group inayomilikiwa na  (UDA)  na kumweleza kuhusu wito huo na akawajibu kuwa angefika mahakamani jana , kitu ambacho hakutekeleza.
Kuhusu mtuhumiwa mwingine, Kiula alidai kuwa, wito wa kufika mahakamani  ulipokewa na kusainiwa na mkewe .Lakini akasema kuwa Yusuph amekuwa hapatikani  kwa simu na kwamba imekuwa vigumu kumpata ofisini kwa kuwa anahisi anahamahama benki.
Baada ya kutoa maelezo hayo hakimu aliridhia na kutoa hati ya kuwakamata kama ilivyoombwa na wamiliki wa takukuru.
Kiula alidai kuwa, katika kesi hiyo ya kugushi inawakabili washitakiwa hao,  yumo matando ambaye alikuwepo mahakamani na alisomewa shitaka lake.
Katika shitaka lao, inadaiwa kuwa,  Oktoba 18, 2009 wakiwa jijini Dar es Salaam, watu hao walidhamiria kughushi hati ya malipo namba 346 ambayo ilikuwa ikionyesha  kuwa chama cha ushirika  cha shinyanga (1984) Limited kilisambaza tani 1,000 za mbegu za pamba zenye thamani ya shilingi 45 milioni wakati wakijua kuwa ni uongo.
Matondo alikana shitaka hilo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wake bado haujakamilika na Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo hadi Julai 28, 2015 .
Mshitakiwa huyo alishidwa kukamilisha mashariti ya dhamana na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kutoa Shilingi 20 milioni.

No comments :

Post a Comment