Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Visiwani Zanzibar, Salum Mwalimu jana aliongelea kuhusu mapokezi ya Lowasa CHADEMA na kugusia kuhusu tetesi za Lowasa kuchukua fomu ya uraisi na kusema haya;
"Tunashukuru sana Watanzania, sidhani kama kuna kiongozi wa CHADEMA simu yake iliwahi kuzidiwa kama jana, simu zilizidiwa kwa pongezi, Kila mtu amezungumza kwa sababu ya Historia ya tendo lenyewe"
"Kesho(LEO) Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA… pengine kutakuwa na shamrashamra nyingi itategemeana na Mgombea mwenyewe, akiamua kuja na mdundiko haya… lakini tunaamini kutakuwa na shamrashamra nyingi."
Salum Mwalimu pia alizungumzia sababu za viongozi wengine wa UKAWA kutokuwepo( Tundu Lissu na Dr. Slaa) ambapo alisema;
"Tuna mambo mengi tuna mikakati mingi, tumegawanyika… sio kila tukio wote tuwe pamoja.
"Jana mliuliza Tundu Lissu yuko wapi na leo huyu hapa hata hamumuulizi… Tuko kwenye kipindi cha Uchaguzi,tuna mambo mengi hatuwezi wote kuwa sehemu moja, tunagawanyika kutokana na ratiba tuliyonayo."

No comments :
Post a Comment