Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara maarufu Jijini humo Juma Mahende, anayemiliki Mabasi ya J4 kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili na kuwapotezea maisha, katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato Jijini humo.
Tukio hilo lilimetokea majira ya saa nne usiku wa kuamkia jana katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato, baada ya mtuhumiwa Juma Mahende kumuita Marehemu Cloud Skalwanda, na mwenzake Ally Mohamed mkazi wa kata ya Igoma kuzungumza masuala ya kibiashara.
Chanzo cha mauaji hayo kikielezwa kuwa marehemu hao walikuwa wakimdai mtuhumiwa shilingi milioni 25/=.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo, amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi mkoani hapa, linamshikilia mtuhumiwa Juma Mahende kwa uchunguzi zaidi.
No comments :
Post a Comment