Sunday, July 5, 2015

UKISTAAJABU YA MUSA, HAUTAYAONA YA KWENYE SWIMMING POOL

 
 
Na. Mwandishi wetu wa Mazingira
 

Utangulizi 

Mara nyingi watu huwa wanavutiwa sana na maji ya bluu yanayong'aa kwenye swimming pool. Lakini unafahamu ni kitu gani unakipata unapoamua kuyasogelea na ku-dive kwenye hizo swimming pool?
 
Duniani kuna watu wa kila aina. Kuna watu wengine huwa wanapenda kujaribu na kuona nini kitatokea baada ya hapo. Na kati ya hawa wanaopenda kujaribu kuna waungwana na wasiokuwa waungwana.
 
Labda tujiulize katika kundi hili la watu wanaopenda kujaribu wasiokuwa waungwana, hakuna hata mmoja ambaye ataamua kujaribu ku-jisaidia haja ndogo au hata kubwa akiwa ndani ya swimming pool?

 "Nakuachia hilo swali ulijibu mwenyewe"
 

Binafsi mimi huwa sipendi kuogelea kwenye swimming pool, hata kama nitaonekana mshamba potelea pote. Nakumbuka kuna siku moja nilikua Mkoani Manyara kwenye sehemu moja maarufu. Kama unavyofahamu mkoa wa Manyara ni mkoa ambao bado ni mpya, hivyo sehemu za starehe ni chache sana. Kwahiyo hiyo sehemu tuliyoeda ndiyo sehemu ambayo ilikua na swimming pool na ndo watu wengi hupenda kwenda hapo. Kwakweli kwa jinsi nilivyoiona ile swimming pool na watu walivyokuwa wengi, nilijionea huruma afya yangu ingawa nilionekana mshamba mbele ya "washikaji" . Nahili ndilo limenifanya niandike makala hii ya leo ili walao niwape uelewa WA-TZ wenzangu.


"Declaimer: Hapa siyo Manyara tafadhali bali nimeonyesha jinsi gani swimming pool zinaweza kujaza watu wengi na hivyo kuona ni jinsi gani watu wanajihatarisha"
Nataka tuongelee "REALFACTS". Unajua ni kwahali gani unajihatarisha unapoenda kuogelea kwenye hizo swimming pool? Je, unajua ni kitu gani hasa kinapatikana kwenye hizo swimming pool. Embu twende pamoja;
 
Watu wengi sana huwa wanaamini kwamba maji ya kwenye swimming-pool ni safi na salama kwa kuwa yamewekewa Chlorine. Wazungu wanasema " sterile". Ukweli ni kwamba hii siyo kweli hata kidogo. Maji ya kwenye swimming pool SIYO MASAFI NA SALAMA, yanaweza kuwa masafi na salama iwapo hakuna mtu aliye ingia kwenye hiyo swimming pool. Narudia tena kwa herufi kubwa "YANAWEZA KUWA SAFI NA SALAMA IWAPO HAKUNA MTU ALIYEINGIA AU KU-DIVE KWENYE HIYO SWIMMING POOL"
 
 Katika mahojiano Bwana Thomas Lachocki, PhD kutoka National Swimming Pool Foundation anasema "Mtu anapoingia kwenye swimming pool maji hayo hayatakua tena safi na salama kama watu wanavyofikiri kwa sababu kuna bakteria hatari wanaoweza kuingizwa na binadamu kwenye swimming pool" . Bakteria hao na vijidudu wengine kutoka kwenye miili ya watu, wanauwezo mkubwa wa kuhimili chlorine iliyopo kwenye maji ya kwenye swimming pool.
 
Bwana  Lachocki anaendelea  kusema kwamba Bacteria watokao kwenye mkojo ni hatari zaidi, na ndiyo maana waogeleaji wengi huwashwa na macho nasehemu zingine za mwili pamoja na machoyao kuwa mekundu. Kuwashwa huku hakusababishwi na chlorine peke yake bali hutokana na " reactions" kati ya mkojo na chlorine. Kuna wengine huwa wanajidanganya kwa kunusa maji ya kwenye swimming pool.

Wengi hujipa matumaini kwa kusikia harufu kali ya maji. Ukweli ni kwamba ile harufu kali wakati mwingine husababishwa na " reaction " kati ya Klorini, mikojo, majasho, kinyesi na hata uchafu mwingine kutoka katika miili ya waogeleaji. Ndiyo maana wengine hupata hadi mafua pamoja na kikohozi wakitoka kwenye swimming pool.

"Upo hapo ?"   


Bingwa wa kuogelewa wa Olimpic wa Marekani anayejulikana kwa jina la Michael Phelps amekiri kwamba yeye na waogeleaji wenzake hwa wana-jisaiadia haja ndogo (hukojoa) ndani ya swimming pool kwa sababu anaamini kwamba klorini huua vijidudu.
 
" Kwahiyo ujinga huu unaonekana hufanywa na watu wengi, ata wazungu, kama ulikua haufahamu nafikiri sasa hivi upo katika position ya kuwashauri wengine hata huyo Michael Phelps kwani yeye ndo nani?"

 
 
Chlorine inapokutana na mkojo na uchafu mwingine, hupoteza uwezo wake wa kupambana na bacteria na vijidudu wengine. Kwahiyo chlorine inafanya kazi vizuri ikiwa yenyewe peke yake, uchafuzi wowote huifanya chlorine kupoteza nguvu yake kwani chlorine itaanza " ku-react "na uchafu na kuacha vijidudu na bacteria wakipeta.
 
Watafiti kutoka Kituo cha kuzuia na kupambana na maradhi (Centre for Disease Control and Prevention- CDC) wanasema kwamba tafiti zao zinaonyesha kwamba kwa wastani mtu mmoja hutoa  kwenye swimming pool kiasi cha;
  • 0.14 gram za " kinyesi"
  • kikombe kimoja cha mkojo
  • kiasi kikubwa cha jasho
  • na mamilioni ya vijidudu wakiwamo bakteria.


Watoto wadogo hutoa gramu 10 za kinyesi kwenye swimming pool. Kama watoto 1000 wataingia kwenye swimming pool, hii inamaana 10,000 grams za kinyesi zitatoka kwenye miili yao kwenda kwenye swimming pool.
 
Utafiti huu unaonyesha kwamba kwenye swimming pool siyo sehemu salama kabisa ya kuogelea na kufuraia kama wengi wafanyavyo, kwani kuna wenzangu hudiriki hata kuyanywa maji ya kwenye swimming pool wanapokua wanaogelea

    Hatari zingine

Maji ya kwenye swimming pool yanaweza kubeba vijidudu vinavyosababisha magonjwa kama vile E. coli na legionella." E. coli ndiyo chanzo kikubwa cha typhoid, kwa hiyo kama wewe ni mpenzi wa kuogelea usishangae kama unaugua typhoid za mara kwa mara"
 
Chlorine inaweza kuviua hivi vijidudu, lakini iwapo vitaingia mdodomi vikiwa havijafa ata kwa kiasi kidogo vinaweza vikakuletea maradhi.
 
Unatakiwa kufahamu kwamba vijidudu vinavyopatikana kwenye kinyesi cha mtu anaye "endesha" haviwezi kuuliwa na chlorine ata vikikaa kwenye swimming pool kwa siku 10.
 
Mwaka 2012 watafiti waliwachunguza waogeleaji 69 waliokuwa wanaumwa magonjwa yatokanayo na maji machafu " water borne diseases". Kati ya waogeleaji 69 nusu yao walipatikana na walipatikana na vijidudu visivyoathiriwa na chlorine.

Ushauri

Watafiti kutoka (Centre for Disease Control and Prevention-CDC) wanashauri maji ya kwenye swimming pool yawe yanaangaliwa mara kwa mara kiasi cha chlorine na pH level yake kwani vijidudu wengi husababisha kupungua kwa kiwango cha chlorine.
 
" Sijajua swimming pool zetu huwa zinachekiwa mara ngapi, au ndo asubuhi mpaka jioni au ata kesho yake, kwanza sidhani ata kama wana vipimo. Naomba uchukue hatua siku moja uwaulize kama wana rekodi ya majibu ya kiwango cha klorini kilichopo au kwa kwa lugha ya kiingereza- Chlorine Inspection and Testing Results nafikiri jibu lao litakufanya uzimie"
 
Kwa muogeleaji unashauriwa kuoga kabla ya kuingia kwenye swimming pool, ma kuhakikisha hauogelei iwapo unahisi unaumwa.
 
"Sijajua ni wangapi wenye moyo huo wa kuoga kabla ya kuogelea kwani wengi wetu huona swimming pool kama ndiyo sehemu ya kuogea"

Ushauri mwingine wa kitaalamu ni kama ufuatao;

  • Epuka kuacha maji ya kwenye swimming pool kuingia mdomoni mwako na kuyameza.
  • Usikojoe kwenye swimming pool kwani utahatarisha afya yako na ya wenzako
  • Usikae sana kwenye swimming pool, kumbuka kupumzika walao kila baada ya saa moja na kuoga . " Najua hili ni suala gumu kwa wenzangu mliolipia kiingilio cha kwenye swimming pool"
  • Kujifuta maji mara kwa mara na hakikisha taulo zinabadilishwa mara kwa mara
  • Chagua sehemu ya kwenda kuogelea, atleast hiyo sehemu iwe na historia nzuri ya usafi na kuyafanyia vipimo maji yao mara kwa mara.
 

Hitimisho

Waswahili wanasema jifunze uelimike, tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba "Public Swimming Pools" siyo sehemu salama kiafya. Nimeandika makala hii ili kukuonyesha hali halisi ya kile  kilichopoo kwenye swimming pool ukweli ambao pengine usingeupata.  Wengi wetu huwa tunajidanganya na chlorine (Klorini)  inayowekwa kwenye maji ya kwenye swimming pool. Kwakuwa nimeshakuelimisha ni jukumu lako kufanya maamuzi sahihi katika kuilinda afya yako.

No comments :

Post a Comment