Na. Emanuel Cosmas
UTANGULIZI
Jamu ya nanasi ni bidhaa inayotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mananasi yaliyosagwa (pulp) na kuchemshwa pamoja na sukari na acid. Ili kupata jamu yenye ubora mzuri ni sharti kuzingatia uwiano mzuri kati ya acid, sukari na pectin.
Mahitaji/Viambaupishi:
Nanasi |
Sukari |
citric acid (Kutegemeana na aina ya matunda) |
Vifaa:
|
·
Sufuria
|
·
Kijiko cha chai
|
|
·
Visu
|
·
Kipima joto (thermometer)
|
|
·
Chujio
|
·
Mwiko
|
|
·
Ndoo
|
·
Sinia
·
Refractometer
|
|
·
Mzani
|
·
Mashine ya kusaga matunda (blender)au ‘pulper’
|
|
·
Ubao wa kukatia matunda
|
|
Hatua za uzalishaji
- Osha matunda vizuri kwa maji safi na salama. Chagua matunda yalyoiva
- Menya matunda na ondoa macho na moyo wa katikati, katakata vipande na uvizage.
- Chemsha kupata pulp ya matunda
- Weka sukari
- Weka acid
- Changanya vizuri, pika polepole ukikoroga hadi joto la kutosha litakapofikia.
- Hakikisha jamu yako imeiva vizuri
- Jaza kwenye chupa safi ikiwa bado ya moto.
- Jamu tayari
END.
Post nzuri, lakini hukusema sukari kiasi gani na citric acid kiasi gani. Nieleweshe hapo
ReplyDelete