Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo katika viwanja vya
Mwembeyanga jana amewataja watanzania walioficha mabilioni ya Fedha katika
Benki za nje ya nchi.
Akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es salaam Zitto
Kabwe amesema hivi sasa uchumi wa nchi umeshikwa na watu wachache hususani
wafanyabiashara ambao pia wameshika siasa au kwa wao kushiriki kwenye siasa moja
kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea maslahi yao.
Ameongeza kuwa nchi ina Kansa ya Ufisadi ambapo watu
hutumia nafasi zao za uongozi kujilimbikizia mali ikiwemo viongozi walioshika
madaraka ya umma.
Mwezi Novemba mwaka 2012 Bunge lilipitisha Azimio namba
Tisa la Mwaka 2012 ambalo lilielekeza Serikali kufanya uchunguzi kuhusu
Watanzania na makampuni ya kitanzania waliotorosha na kuficha fedha kwenye
mabenki ughaibuni.
Uchunguzi pia ulikuwa uhusike na Mali za Watanzania
zilizopo nje ya nchi katika juhudi za kuhakikisha kuwa fedha chafu na ufichwaji
wake vinakomeshwa. Bunge lilitoa muda wa miezi sita kwa Serikali kufanya
uchunguzi huo.
Mwaka mzima ulipita Serikali haikutoa maelezo yeyote na
baada ya kubanwa ndani ya Bunge Serikali ikaomba miezi sita zaidi. Hata hivyo
mpaka leo Serikali haijatoa kauli yeyote kuhusu taarifa hiyo ya
uchunguzi.
Ametolea mfano kuwa taarifa ya Serikali ya kisiwa cha
Jersey kilicho chini ya himaya ya Uingereza inaonyesha kuwa Fedha na Mali za
Watanzania katika mabenki kisiwani humo ni paundi za Uingereza 440 milioni
ambazo kwa bei ya sasa ni sawa na shilingi za kitanzania 1.4
trilioni.
Vile vile taarifa rasmi ya Benki Kuu ya Uswiss
inaonesha kuwa Watanzania wenye akaunti katika mabenki ya nchi hizo imefikia
dola za kimarekani 304 milioni kutoka dola 213 milioni mwaka 2012. Amesema hana
takwimu kwa nchi nyingine duniani huku akisistiza kuwa fedha hizi zilizofichwa
zaweza kuwa halali au haramu.
Amesisitiza kuwa Serikali imenyima haki hiyo kwa zaidi
ya miaka miwili na nusu sasa. Bunge la Kumi linavunjwa mnamo tarehe 9 Julai
mwaka huu na hakuna dalili yeyote ya Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi ndani
ya bunge kama ilivyoagizwa na Bunge.
Orodha hiyo amesema ali iwaslisha kwa Gavana wa Benki
Kuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
kwa ajili ya uchunguzi lakini Serikali mpaka sasa haijatoa taarifa licha ya
kupewa kila aina ya ushirikiano.
“Nimeamua leo kuiweka orodha hii wazi kama shinikizo
kwa Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki
ijayo.”Amesema Zitto
Orodha hiyo ina majina 99 ya Watanzania au watu wenye
mahusiano na Tanzania ambao wana akaunti HSBC ya Uswiss. Jumla ya akiba katika
akaunti Benki hii pekee ni dola za kimarekani 114
milioni.
Orodha hiyo ipo kama inavyoonekaa hapo chini:
No comments :
Post a Comment