HATIMAYE Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa leo amerejesha fomu ya kuomba uteuzi
kuomba urais kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Aidha, katika urejeshaji wa fomu Lowassa amepata udhamini kutoka mikoa 32 ambao amedhaminiwa na wanachama zaidi ya milioni 1.6
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Organaizesheni na Uchaguzi, Benson Kigaila amesema, wadhamini hao wamepatikana kutoka katika Kanda 10 na Mikoa 32 kwa nchi nzima.
“Sasa safari ya matumaini kupitia CCM imeishia njiani,safari ya uhakika kupitia Chadema imefika na kipindi hiki lazima kieleweke na tunaenda kuiondoa CCM madarakani asubuhi kweupe”,amesema Kigaila.
Ameongeza kuwa wanachama kutoka mikoa yote walikuwa wakitamani Lowassa apitie mikoa yote ili kumdhamini kutokana na muda mchache wameamua kumdhamini kupitia njia ya simu.
Kigaila ambae pia ni Mkurugenzi wa Kanda wa Mambo ya Uchaguzi wa chama hicho amesema wanachama wasijali chochote kwa kuwa baada ya mkutano mkuu kumpitisha mgombea ambao unatarajia kufanyika Agosti nne atachanja mbuga kuzunguka mikoa yote.
Nae Profesa Abdallah Safari ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara amesema amemshukuru Lowassa kwa kurejesha fomu hiyo kwa kuwa baadhi ya watu walidhani angeingia mitini kwa hiyo sasa tunajiandaa kwenda kuchukua dola.
Nae Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu amesema chama tawala hawawezi kuwasambaratisha chadema na kuja kwa Lowassa ni mpango wa mungu na nyama zote walizopanga hazitafanikiwa.
No comments :
Post a Comment