Thursday, August 6, 2015

WWII: MADHILA YA SHAMBULIO LA HIROSHIMA NA NAGASAKI

Battle: Lewis Philbrick, 86, says he requested meetings with MoD bosses for years about his cancer but has been snubbed
Raia wa Japan leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima.
Lewis Philbrick escorted scientists to the site of the Nagasaki atom bomb after it was dropped in 1945
Lewis Philbrick enzi za ujana wake
Lewis Philbrick (Picha ya mwanzo) ni moja kati ya wanajeshi wa Marekani aliyewasindikiza wanasayansi waliotumwa nchini Japani kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kilichotokea mwaka 1945 mwezi mmoja baadae ya kudondoshwa kwa bomu hilo. Mara baada ya kufika Japani alianza kutoka damu kwenye fizi, na kuvimba lipsi na alibainika kuwa na kansa mwaka 1984.
Uso wake ulifanyiwa operation mara 7 ambapo asilimia kubwa ya taya lake na fuvu la kichwa viliondolewa. Kwa sasa Philbrick amesema hataki fidia yeyote isipokuwa anataka kutambuliwa kwamba alijitoa.

Anasema; "Siwezi sahau kwakuwa kila ninapojiangalia kwenye kioo naliona tukio na huwa napata wasiwasi kwamba ni lini itatokea tena"


B-29 Ndege iliyodondosha bomu la atomic
              
Takriban watu laki moja na arobaini walikadiriwa kupoteza maisha baada ya Ndege ya Marekani kudondosha bomu ambalo liliuharibu mji huo tarehe 6 mwezi Agosti mwaka 1945.

Bomu la Atomic lililodondoshwa na ndege vita ya marekani ya American B-29 bomber katika mji wa  Hiroshima. Mripuko uliangamiza asilimia 90 ya mji na kuuwa watu 80,000  hapo hapo na wengine 10,000 walikufa baadae kutokana na mionzi.
.

Siku tatu baadae  shambulio jingine la bomu la Atomiki lilifanyika katika mji wa Nagasaki ambapo watu 40,000 walikufa papo hapo. Kiongozi wa Japani kwa wakati huo aliamua kutangaza nchi ya Japani kushindwa vita vya pili vya dunia mnapo tarehe 15 mwezi wa nane.

Japan ilijisalimisha siku kadhaa baadae, hatua iliyomaliza vita ya pili ya dunia.
Kusainiwa kwa makataba wa kusitisha vita ya pili ya dunia

Imeandaliwa na: Emanuel

No comments :

Post a Comment