Watalamu kutoka Ufaransa, Malaysia na Australia wameanza kuchunguza mabaki ya bawa la ndege iliyopatikana juma lililopita likiwa limesombwa hadi ufukweni na maji ya bahari Hindi katika kisiwa cha Re-Union karibu na Madagascar.
Nia hasa ni kubaini iwapo mabawa hayo ni sehemu ya mabaki ya ile ndege ya Malaysia ya MH370, iliyotoweka
Sehemu iliyoshikana na ndege pia inachunguzwa ili kujua ilimeguka kutoka wapi. Ndege hiyo ya MH370, ilitoweka angani mwezi Machi mwaka jana ikiwa na abiria 239 na wahudumu wa ndege.
No comments :
Post a Comment