Kwa mujibu wa sheria ya chakula na madawa ya mwaka 2006 (TFDA, Food drug and cosmetic (Food labeling regulation, 2006) mtu yeyote haruhusiwi kuuza chakula
kilicho tengenezwa, kusindika, au kufungashwa bila ya kuwa na label.
Na mtu yeyote atakayeshindwa kutimiza hili basi anavunja sheria hii na anapaswa kuchukuliwa hatua na anapaswa kutozwa fine isiyozidi elfu hamsini au kifungo kisichopungua miezi sita.
Label nyingi za vyakula kwa hapa nchini kwetu huwa zinakosa ubora. Ubora wa label siyo picha zinazowekwa kwenye label au urembo mwingine bali ni ;
- taarifa muhmu zilizopo kwenye label husika
- uwezo wa kusomeka na kueleweka na
- uwezo wa label kukaa kwenye kifungashio husika kwa muda mpaka bidhaa inapotumiwa au kutumika.
Ili label iweze kuwa na maana ni lazima itoe taarifa mbalimbali zikiwemo taarifa zinazohusiana na ubora na usalama wa chakula husika. Taarifa muhimu zinazotakiwa kuwekwa kwenye label ni hizi zifuatazo;
i.Jina la bidhaa iliyofungashwa
ii.Vilivyomo (ingredients)
iii.Uzito/ujazo
iv.Jina na anuani ya mtengenezaji
v.Tarehe ya kutengeneza
vi.Tarehe ya mwisho wa matumizi.
vii.Jina la biashara au nembo
viii. Nembo muhimu (TBS kwa wale wenye uhakiki, trade mark n.k.)
ix. Namba ya toleo (Batch Namba).
Muhimu:
Taarifa zinazowekwa kwenye label ya chakula zinatakiwa ziwe ni za kweli, kwa mujibu wa sheria ya chakula na dawa ya mwaka 2006, kuweka taarifa za uwongo kwenye label ni kuvunja sheria na mtu anayefanya hivi anapaswa kuchukuliwa hatua.
No comments :
Post a Comment