Ripoti nyingi zilizotoka mwaka 2000 zimedhibitisha kwamba wine nyekundu zinafaida kubwa kiafya hasa kusaidia katika kupambana na magonjwa yanayohusu mzunguko wa damu na magonjwa ya moyo.
Mnamo mwezi wa tisa ripoti iliyotolewa na watafiti wa Sweden kwenye taasisi ya Karolinska imedhibitisha kwamba unywaji wa kistaarabu wa wine husaidia kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na kansa.
Katika matokeo ya utafiti yaliyochapishwa mwaka 2000 katika jarida liitwalo journal Pharmacology, Biochemistry, and Behavior yalieleza kwamba katika mji wa Amsterdam wanaume na wanawake 275 wenye umri wa miaka 32 waliokuwa wanapewa glasi moja au mbili kwa siku walikutwa na kiwango kidogo cha cholesterol mbaya mwilini.
WINE NYEKUNDU HUSAIDIA KUZUIA KANSA
![](https://edc2.healthtap.com/ht-staging/user_answer/reference_image/4932/large/BPH.jpeg?1386670455)
Ripoti iliyoandikwa kwenye jarida liitwalo American Journal of Epidemiology na kuchapishwa mwaka 2000 linaonyesha kwamba wanawake wanaokunywa gramu 11 hadi 20 kwa siku, sawa na glasi moja hadi tatu za wine, wamegundulika kuwa na kiwango kikubwa cha madinini na mifupa yenye afya zaidi ya wale wasiotumia au wanywaji waliopitiliza.
UNYWAJI WA KISTAARABU UNAFAIDA
Afya ya moyo, ulinzi dhidi ya kansa na uimara wa mifupa na faida zingine zinaweza kupatikana iwapo kutakuwa na unywaji wa kistaarabu.
![](https://grapecollective.com/media/wysiwyg/michelle-and-barack-obama-red-wine-lover.jpg)
Kwa sasa mado kuna mkanganyiko kuhusiana na definition ya "unywaji wa kistaarabu mpaka pale wataalamu na watafiti watakapo kuja na maana kamili ya kiwango sahihi, lakini bado unaweza kudhibiti unywaji wako kwa kuhakikisha hauzidishi zaidi ya glasi mbili za wine kwa siku kwa wanaume na glasi moja kwa wanawake.
No comments :
Post a Comment