Ishu ya ESCROW ni kama kuna watu wengi walianza kuisahau hivi. Jana imerudi tena kwenye masikio ya watu ambapo tunakumbuka kuna orodha ya Mawaziri na Wenyeviti wa Kamati za Bunge walisimamishwa baada ya kutajwa kuhusika na mgao wa Bil. 300 zilizokuwa kwenye account ya ESCROW.
Mbunge Andrew Chenge alikuwa mmoja ya waliotajwa
kuhusika pia, ishu ikapelekwa Kamati ya Maadili na baadae Mbunge huyo akapeleka
ombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ili kuzuia kuhojiwa na Kamati
hiyo.
Jana June 26 2015 ripoti kutoka Mahakamani inasema Mahakama hiyo imetupilia mbali Ombi hilo kwa kuwa imeona haikuwa na Mamlaka ya kuzuia Shauri hilo, na walichokiona ni kwamba Chenge alikuwa na njia mbadala kushughulika na ishu hiyo badala ya kukimbilia Mahakamani

No comments :
Post a Comment