Siku chache zimepita tangu hukumu ya kesi ya Mbunge wa
Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kutolewa dhidi ya mzazi mwenzake Faiza
Ally,baada ya kuiomba mahakama kumchukua mtoto wao, hali iiyopelekea mahakama
kutoa hukumu kuwa mtoto achukuliwe na Mbunge huyo, jambo lililofanya sakata
hilo kutinga bungeni.
Baadhi ya wabunge na wadau mbalimbali wamedai kuwa
mtoto bado ni mdogo sana kuweza kuishi na baba yake na kutoa maoni kuwa mtoto
arudishwe kwa mama yake kwa kuwa kila mtu ana mapungufu na kusema kuwa mtoto
bado ana haki ya kuwa karibu na mama yake.
Kwa mujibu wa Mbunge Martha Mlata jana alisema kuwa;
“Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja
Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu
mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake”.
Hoja hiyo ikachangiwa na Mbunge David Kafulila alisema
“Hii nchi ina mihimili mitatu, Bunge, Mahakama na Serikali… Tuheshimu maamuzi
ya Mahakama”.
Sambamba na hilo Waziri Saada Mkuya akahitimisha na
kusema; “Kama mama na mimi nilipoisikia ile taarifa nilipata uchungu, kila
binadamu ana mapungufu yake lakini mtoto alelewe na mama
yake”.
No comments :
Post a Comment