Baada ya kuchukua fomu hiyo jana, Sonoko alisema kama
chama hicho kitampitisha kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na
kushinda, moja ya vipaumbele vyake ni pamoja na kuzingatia misingi imara ya
ilani ya 2005 pamoja na kuondoa umaskini kwa Watanzania.
Sonoko amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke ambapo katika kampeni zake za kusaka
urais atatumia kauli mbiu inayosema "Kutokomeza Umaskini".
Alisema akiingia Ikulu, atawatimizia Watanzania
mahitaji mbalimbali ambayo wameyakosa muda mrefu ambapo yeye ana sifa zote za
kuwa rais ndio maana ameamua kuchukua fomu.
Aliongeza kuwa atahakikisha nchi inaendeshwa kwa kodi
za wananchi si misaada kutoka nchi wahisani ambapo wanawake watawezeshwa katika
mambo mbalimbali na kupewa nyadhifa kwenye vyombo vya maamuzi pamoja na
vijana.
Sonoko alisema Serikali ambayo ataiongoza itasimamia
haki, kupinga vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa hasa Mahakamani ambapo kesi
zitakuwa zikiendeshwa kwa muda maalumu, kurudisha viwanda, kuinua kilimo na
kuboresha miundombinu.
"Nitahakikisha kila Wilaya inakuwa na sehemu yake ya
kuegesha magari, kuongeza ajira na kuwasaidia vijana," alisema na kuongeza kuwa,
hadi Julai mosi, mwaka huu, atakuwa amekamilisha taratibu za kupata wadhamini
450 katika mikoa 15.
No comments :
Post a Comment