Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa
kauli moja imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar
kupitia chama cha mapinduzi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa
Zanzibar wanounda kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi
kuu ya CCM na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena kiti hicho cha urais
baada ya wajumbe karibu 102 ambao ni aslimia 83 kuridhia Dr Shein
agombee.
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM
Zanzibar alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao
ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu wa
rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein aliwahidi
wanachama wa CCM kuwa uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza ilani ya CCM ya
kuitumikia Zanzibar.
Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar
akizungumza baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala
la majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote
utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo mapya leo
asubuhi.
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na
kamati maalum ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo
jina la Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na
kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar inaamuliwa na
NEC na siyo na mkutano mkuu wa-CCM
No comments :
Post a Comment