Wednesday, July 8, 2015

LAPTOP YA BVR YAIBWA

Picha kutoka maktaba
Kompyuta mpakato (laptop) inayotumika kwenye mashine ya ‘Biometric Voter Registration’ (BVR) imeibiwa na watu wasiojulikana katika Kata ya Nyugwa wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.

Akisimulia tukio zima lilivyokuwa, Afisa mwandikishaji msaidizi wa uchaguzi wa halmashauri ya
 
Nyang’hwale Slyvester Kabora, alisema kuwa mashine zote za BVR zilikaguliwa na kuonekana ziko salama ambapo zilipakiwa kwenye gari na hatimaye maafisa uandikishaji walikabidhiwa lakini cha kushangaza walipata taarifa mashine moja imenyofolewa laptop mpakato.

Alisema Kifaa hicho kiliibiwa mnamo Julai 6 mwaka huu, ambapo maafisa uandikishaji waliofika katika kituo zilipokuwa zimehifadhiwa mashine hizo saa 12:00 asubuhi, waligundua mashine moja ina kasoro.

“Mashine zile zilifikishwa katika kata ya Nyugwa zikawekwa katika ofisi za kata hiyo, ila cha ajabu asubuhi maafisa wakiwa katika harakati za kuzisambaza mashine hizo kwenye vituo ndipo moja iligundulika haina laptop... lakini mazingira ya kuibiwa laptop hiyo ni ya kutatamisha kwa sababu mlango ulikuwa haujavunjwa" 
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Fortunata Mallya alikanusha madai ya kuwa mashine moja ya BVR imeibiwa kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyo ripoti.

Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake Fortunata Mallya alisema kuwa kuna redio moja nchini (jina tunalo), ilitangaza kuibiwa kwa mashine hiyo taarifa ambazo ni za uongo na kwamba kitu kilichoibiwa kwenye mashine hiyo ni laptop na siyo mashine ya BVR.
“Nimesikitishwa sana na baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari pasipo kujiridhisha kama taarifa hizo ni za kweli ama la. Kwanza nawashukuru sana nyinyi waandishi mliofunga safari kutoka Geita kuja huku kufuatilia suala hili, ni kwamba nina mashine BVR 49 moja ndiyo waliyoitolea laptop,’’
 Watu watatu wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo ambao ni Aloyce Kata mkazi wa eneo hilo, wengine wawili majina yao hayakuweza kufahamika mara moja.
 

No comments :

Post a Comment