WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.
Waliokufa ni Chacha Mwita (24) aliyechomwa kisu kifuani
na mwenzake wakigombea mwanamke wa baa huko Sirari.
Wengine ni Juma Nguka (25) aliyeuawa na watu wenye
hasira baada ya kutuhumiwa kupora pikipiki yenye namba za usajili MC 936 ACA,
mali ya Erick Jumanne mkazi wa Kijiji cha Mkoma.
Tukio lingine ni kufa maji kwa mvuvi aliyefahamika kwa
jina la Wambura Maregeri (30) mkazi wa kijiji cha Muhundwe aliyekufa maji baada
ya Boya kutoboka.
Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP Swetbert
Njewike alisema kuwa matukio hayo matatu ya vifo yalitokea Julai mosi mwaka huu
katika Wilaya za Rorya na Tarime.
Akielezea tukio la baa ambalo Mwita aliuawa, alisema
siku hiyo marehemu akiwa baa moja katika mji wa Sirari, Tarime, nyakati za saa
moja jioni kulitokea ugomvi kati ya marehemu na mtu mwingine ambaye hajafahamika
jina lake wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la
Dina.
Alisema wakati wa ugomvi huo, Mwita alichomwa kisu
kifuani na aliyefanya kitendo hicho alitoroka ambapo majeruhi huyo alitokwa damu
nyingi na alipofikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime alifariki
dunia.
Alisema Nguka yeye alipoteza maisha baada ya
kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuiba
pikipiki.
Akasema Maregesi alikufa maji baada ya boya lililotengenezwa kienyeji alilokuwa anatumia katika uvuvi kutoboka na kuzama majini hali iliyopelekea kifo chake.
Akasema Maregesi alikufa maji baada ya boya lililotengenezwa kienyeji alilokuwa anatumia katika uvuvi kutoboka na kuzama majini hali iliyopelekea kifo chake.
“Jeshi la Polisi linafanya msako wa watuhumiwa wa
mauaji Chacha Mwita na watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya Nguka ili waweze
kufikishwa katika vyombo vya Sheria,” alisema.
No comments :
Post a Comment