Rukwa: POLISI mkoani Rukwa imewakamata watuhumiwa 19 na silaha za aina mbalimbali zikiwemo bunduki 30, risasi 231 pamoja na mtambo wa kutengeneza bunduki za kienyeji.
Katika msako uliofanywa na Polisi mkoani hapa, pia
waliweza kukamata nyara za Serikali yakiwemo meno, mikia miwili ya tembo na
maganda mawili ya risasi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda
alisema jana mjini hapa kuwa silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni ya
kupambana na visa vya ujangili na uhalifu mwingine katika maeneo mbalimbali
ndani ya mkoa huu.
Alibainisha kuwa silaha hizo zilizokamatwa zinasadikiwa
kutumika katika visa vya kijangili na uhalifu mwingine ambapo baadhi ya bunduki
zimegundulika kuwa zinamilikiwa kihalali.
Alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni bunduki aina ya
shotgun 8, rifle 8, magobori 4, bunduki 6 aina ya shotgun zilizotengenezwa
kienyeji, risasi 5 za SMG, risasi 53 za rifle na risasi 173 za
shotgun.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda watuhumiwa hao
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa awali wa
kukamilika.
No comments :
Post a Comment