Friday, July 31, 2015

TAARIFA KUHUSU ACOUNT FAKE ZA TWITTER NA FACEBOOK

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA JAMII



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa kunawatu wanatumia jina la TANESCO vibaya katika mitandao ya kijamii (facebook na twitter) kujibu watu matusi, kulikashifu Shirika na kutoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu Shirika kwa kujifanya wao ni TANESCO.

Shirika limeshatoa taarifa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuwasiliana na vyombo vingine vya usalama juu ya uhujumu huo. Mitandao hiyo ina akaunti za facebook zinazosomeka (TANESCO TZ na TANESCO) na akaunti za twitter zinazosomeka (Tanesco @TANESCO-, Tanesco Escobar @tanescobar, TANESCO LTD @tanesco-)

TANESCO inaendelea kuzikana akaunti hizo na kwamba chochote kinachoandikwa huko si msimamo au maelezo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Mitandao sahihi ya Tanesco ni Facebook: www.facebook.com/tanescoyetu Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Uongozi unaomba radhi wateja wake kwa usumbufu wowote walioupata kutokana na upotoshwaji wa taarifa kwenye mitandao hiyo.

Imetolewa na:


OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.

No comments :

Post a Comment