TAARIFA YA UBORESHAJI WA MFUMO WA LUKU
Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) linafuraha kuwajulisha wateja wake kote
nchini wanaotumia mfumo wa LUKU kwamba kuanzia Agosti 1
mwaka huu tutahamia kwenye mfumo mpya wa LUKU
ulioboreshwa zaidi. Mfumo huo ambao
umeboreshwa utakuwa na kasi zaidi, utaweza kuhudumia idadi kubwa ya wateja
kwa wakati mmoja na utaondoa usumbufu wowote ambao ulijitokeza kwenye
mfumo wa awali.
Hivyo
wakati wa kuhamia kwenye mfumo huo mpya tutasitisha huduma ya kununua umeme kwa wateja wa LUKU usiku wa kuamkia Agosti 1, 2015 kwa
muda wa saa 24.
Uongozi unaomba radhi kwa
usumbufu wowote ambao unaweza kujitokeza.
TANESCO:
“Tunayaangaza Maisha Yako”
Imetolewa
na: Â OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.
No comments :
Post a Comment