Sunday, July 5, 2015

WABUNGE WENGINE 35 WAPIGWA "STOP" KUINGIA BUNGENI KWA SIKU TANO KUANZIA JANA TAREHE 4, 2015

Dodoma: Hali ya fukuza fukuza Bungeni imendelea tena siku ya jana ambapo wabunge wapatao 35 walisimamishwa kwa siku 5 mfululizo kutohudhuria Vikao vya bunge. Hali hiyo ilitokea kutokana na kile inachoonekana ni kukosekana kwa maadili kutokana na kuzuka kwa kelele kutoka kwa wabunge wakati wa uchangiaji wa miswada. 
 
Kwa siku ya jana, tarehe 04, 2015 Kikao kilianza tena saa tatu asubuhi. Mbunge Ezekiel Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?

Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele, kutokana na hilo Spika akataja "list" ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku tano kila mmoja.

 Wabunge hao ni;

Ezekiel Wenje

Mussa Kombo

Masoud Abdallah Salim

Rebecca Ngodo

Sabrina Sungura

Khatib Said Haji

Dr. Anthony Mbassa

Maulidah Anna Valerian Komu

Kulikoyela Kahigi

Cecilia Pareso

Joyce Mukya

Mariam Msabaha

Grace Kiwelu

Israel Natse

 Mustapha Akonaay

Konchesta Rwamlaza

Suleiman Bungura

Rashid Ali Abdallah

Ali Hamad

Riziki Juma

Rukia Kassim Ahmed

Azza Hamad

Khatibu Said Haji

Kombo Khamis Kombo

Ali Khamis Seif

Haroub Mohammed Shamisi

Kuruthum Jumanne

Mchuchuli

Amina Mwidau

Mkiwa Kimwanga

Salum Baruhani

Marry Stellah Malaki

Rashid Ally Omary

Mwanamrisho Abama

Lucy Owenya


Tujikumbushe


Siku ya Alhamisi July 02, 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kujadili Miswada mitatu kwa siku moja, kwakuwa ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge. Kutokana na hilo ukatokea mvutano na baadae Spika Anne Makinda akaahirisha Bunge.


Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyohivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.


 

 

No comments :

Post a Comment