Watu watano, akiwemo mfanyakazi wa NMB wanashikiliwa na polisi kutokana na kuhusishwa na wizi wa mil 200 katika benki ya NMB tawi la Mkuranga mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Pwani-CP, Jafari Ibrahim, watu wane kati yao ni walinzi waliokuwa wanafanya kazi katika kampuni binafsi ya ulinzi iliyopewa jukumu la kusafirisha fedha kutoka Dar es salaam kwenda Mkuranga-Pwani.
Kamanda wa poilisi ameongeza na kusema kwamba, mtuhumiwa mwingine aliyekamatwa ni mfanyakazi wa NMB ambaye jina lake na cheo chake vinahifadhiwa, na anaendelea kuhojiwa na polisi.
Majambazi watatu waliokuwa na silaha aina ya SMG walivamia na kuua polisi mmoja na kujeruhi watu wawili katika tukio lililotokea tare 26 mwezi wa sita, kaba ya kupora pesa zaidi ya mil 200 katika benki ya NMB tawi la Mkuranga. Tukio hilo lilitokea mda mchache baada ya kuwasili kwa fedha kutoka Dar es salaam. Katika siku ya tukio, majambazi walimuua afisa polisi mmoja ambaye hakuwa katika zamu siku ya tukio lakini alikua kwenye benki hiyo ambaye alikua anasubiri shifti ya usiku. Watu wengine wawili walijeruhiwa na kuwahishwa katika hospitali . Mpka sasa majeruhiwa wamesharuhusiwa.

No comments :
Post a Comment