Saturday, July 4, 2015

HANGOVER (MNING'INIO)


 
 
  • Utangulizi

Kwamujibu wa Jarida la Habari za Matibabu (Medical News Today); Hangover ni mkusanyiko wa dalili ambazo huusishwa na unywaji wa pombe au vileo, ambao umetokea karibuni. Maranyingi hangover hutokea mara baada ya masaa 24 baada ya kunywa pombe. Mtu mwenye hangover hupata dalili mbalimbali kama vile kuumwa kichwa, kujisikia mgonjwa, kizunguzungu, kujihisi kuchanganyikiwa kujihisi kiu ya maji, n.k.

Hangover inawezekana ikatokea mda wowote, lakini mara nyingi hutokea wakati wa asubuhi mara baada ya usiku wa kula "gambe".
 
 
Licha ya dalili ambazo mtu anazipata na kuzikia mwilini mwake, vilevile hangover humfanya mtu ajisikie hali ya msongo wa mawazo, kujuta, aibu na hata hali ya kujihisi ameaibika au aibishwa.


 

  • Nini kinasababisha hangover?

Kwa mujibu wa Professor Oliver James, Mkuu wa Idara ya Matibabu chuo kikuu  Newcastle University, pombe huzuia utengenezwaji wa homoni inayoitwa "vasopressin", homoni hii hudhibiti kiwango cha maji kinatolewa na figo nje ya mwili kupitia mkojo. Upungufu wa homoni hii hufanya maji mengi kutolewa nje ya mwili, na ndiyo sababu ya watu kukojoa kwa wingi wanapokunywa pombe. Kila lita moja ya pombe hufanya ongezeko la ml 10 za mkojo
 

.Kiwango cha hangover kinategemeana na kiwango cha unywaji au kiasi cha pombe kilichonywewa. Sababu zingine ni muda mtu alitumia kulala. Kama mtu atalala kwa mda mfupi ndivyo atakavyopata " hangover" kwa kiasi kikubwa. Ni vigumu sana kusema ni kiasi gani cha kileo mtu anapaswa kunywa ili asipate "hangover"-suala hili linategemeana na mtu mwenyewe; kwa maan kwamba itategemeana na huyo mtu alikua kwenye hali gani kabla ya kuanza kunywa au kupata kileo. Je, Alikua amechoka kiasi gani kabla hajanza kunywa, alikua na kiasi gani cha maji mwilini kabla hajaanza kunywa, Je alikunywa maji kabla hajanza kupata kileo (vileo) na wakati wa kunywa pombe.

"Kutokana na hili vi vyema kwa mtu kuanza na maji kabla ya kuanza kusukumizia bia au vileo vingine,  na vilevile ni muhimu mtu kunywa maji mengi baada ya kunywa au katikati ya "gambe", hii ni kwa sababu unywaji wa maji utasaidia kurudisha maji  yaliyopotea mwilini kutokana na kupata haja ndogo mara kwa mara"
  • Dalili za hangover


Dalili kubwa za hangover ni kuumwa kichwa au kujihisi kiu ya maji.
Dalili za hangover huanza kutokea pale kiwango cha kileo au pombe kinapoanza kupungua kwenye damu, mara nyingi hali hii hutokea baada ya masaa 24. Kwahiyo itategemeana na mtu alianza kunywa bia au vileo vingine saa ngapi.

Dalili zingine za hangover mi kama zifuatazo;

  • Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
  • Mwili na misuli kuuma
  • Kuharisha
  • Kizunguzungu
  • Kupumua kwa shida
  • Kutokwa na mate mengi
  • Kutoa "hewa chafu"
  • Kichefuchefu
  • Kuwa "sensitive" sana na kelele
  • Kuumwa tumbo
  • Kupoteza mudi "moodiness"
  • Kukosa usingizi
  • Kupata kiu
  • Kutapika
  • Kupungua kwa joto la mwili
  • Mtu kupoteza "network"
  • Mtu kupata msongo wa mawazo "Depression"

  • Jinsi ya kuondokana na hangover

kwa mujibu wa jarida la afya- Health.com njia sahihi ya kuondokana na hangover ni kunywa  pombe "kistaarabu" au kuacha kabisa kunywa pombe au vileo.
 
Njia zingine zinazoweza kutumika ni kuhakikisha unapata maji ya kutosha au kunywa kinywaji kisichokuwa na kileo kila baada ya bia moja au bia kadhaa na kula vyakula vyenye mafuta ili kupunguza kasi ya pombe kuingia kwenye damu au mwilini.
"Nyama choma kwa wingi, ama nini"
Unywaji wa maji husaidia kurudisha mwilini  maji, kwani chanzo kikubwa cha hangover ni mwili kuishiwa maji .
 
"Kwahiyo ukimuona mtu anakunywa maji kila baada ya bia kadhaa usifikiri kwamba hana ela ya bia, mwenzako amegundua siri"





" Siunajua tena mbio za kwenda maliwatoni huwa haziishi wakati wa gambe"


 
 
 

 
Njia nyingine zinaweza kutumika lakini kuna baadhi ya njia zinafanya kazi na zingine huwa hazitoi matokeo ya kweli na wakati mwingine huzidisha hangover.

Baadhi ya njia  ambazo watu wengi wanazitumia ni hizi zifuatazo;

1. Kunywa pombe zingine asubuhi  au kwa lugha ya kigeni -Hair of dog   

 
Njia hii hutumiwa sana na watu  wakiamini kwamba kitendo hicho huondoa hangover. 

Kitaalamu kitendo hichi hakiondoi hangover bali huituliza kwa mda Kama tulivyogusia hapo awali, mtu huanza kuzipata dalili za hangover pale kiwango cha pombe kinapoanz kushuka kwenye damu, kwahiyo unapokunywa bia zingine utakua unaongeza kiwango cha alcohol kwenye damu hivyo kuzisimamisha kwa mda dalili hizo. Dalili hizo huweza kujirudia baada ya masaa au siku kulingana na kiwango cha pombe ulichokunywa na kuifanya hali kuwa mbaya zaidi.

2. Kupata kifungua kinywa chenye asili ya mafuta kama supu

Hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba vya ulaji wa vyakula vyenye mafuta hukata hangover ingawa watu wengi wanatoa ushahidi kwamba supu na nyama hukata hangover. "Wakati mwingine vyakula vyenye mafuta huishia kuwaasababishia watu kiungulia" anasema Dr. Cutler. A nashauri ulaji wa vyakula ambavyo ni rahisi kufanyiwa mmeng'enyo na mwili kama vile vyakula vinavyotokana na nafaka ambavyo anasema husaidia katika kuurudishia mwili nguvu iliyopotea. Mwanasayansi mwingine , John Brick, PhD, ambaye ni mtafiti wa vileo na mwandishi wa kitabu kinachoitwa "The Doctor’s Hangover Handbook" anaamini kwamba kula kidogo na kunywa maji mengi husaidia katika kurudisha maji mwilini nakukata hangover. Anaamini kwamba hakuna vyakula maalumu kwa ajili ya kukata hangover ingawa anamaini sandwiches zenye asali husaidia baadhi ya watu. Ushauri mwingine ni kula matunda kama vile ndizi na apple. Matunda haya yana kiwango kikubwa cha sukari ambayo itasaidia kukurudishia nguvu ulizopoteza. Vile vile matunda haya yana madini kama vile potassium na magnesium. Magnesium hutumika katika kuusaidia mwili " ku-relax" na kusaidi kuondokana na kichefuchefu

3. Kutumia kahawa

Wakati mwingine watu hunywa kahawa ili kukata hangover. Wanasayansi wanasema kwamba matumizi ya kahawa husisimua mwili hivyo husababisha mwili kuhitaji nguvu za ziada. Si hivyo tu pia na mishipa ya damu kusinyaa na kuongeza presha ya damu kitu ambacho husababisha maumivu ya kichwa hivyo kuongeza makali ya hangover.
Hali hii huweza kutokea kwa wanywaji wa "Energy drinks" ambapo kinachotokea mwili husisimka na kuufanya uzalishe kiwango kikubwa cha nguvu " energy" zaidi ata ya kile kiwango kinacholetwa na hivyo vinywaji.

Njia ya rahisi na sahihi ni kunywa chai iliyochanganywa na limao kikombe kimoja au viwili "usizidishe kwani inaweza kukufanya utokwe na haja ndogo nyingi hivyo kukuletea shida tena ya kupungukiwa na maji" 

4. Kufanya mazoezi

Kama mtu anajiweza ufanyaji wa mazoezi unaweza kusaidia kurudisha mwili katika hali yake ya kawaida. Ingawa kwa mtu aliyekunywa pombe kufanya mazoezi baada ya kuamka siyo jambo la msingi, cha msingi zaidi ni kupata mda wa kutosha wa kupumzika

5. Kuoga

Kuoga ni njia mojawapo inayoshauriwa na wataalamu katika kupunguza hangover. Kuoga huusaidia mwili ku-relax . Joto la maji litategemeana na mtu atakavyopendelea kwani maji ya baridi husaidia kuamsha mwili wakati maji ya moto husaidia kuufanya mwili na misuli kurelax. Kwaiyo kama una-system nzuri ya maji unaweza "ku-altenate" kati ya maji ya moto na baridi.
 Maji ya moto sana au mvuke kwa wenye sauna haishauriwi kwani kitendo hicho husababisha kutanuka sana kwa mishipa ya damu na hivyo huweza kuleta shida katika mzunguko wa damu. Watafiti kutoka kampuni ya Utafiti inayoitwa Finnish State Alcohol iliyopo  Helsinki, wanataadharisha matumizi ya Sauna kwamba ni hatari kwa afya, kwani yanaweza sabaisha kushuka kwa presha ya damu na mabadiliko katika mapigo ya moyo kutokana na kutanuka kwa mishipa ya damu.
 

6. Kulala

Kupata muda wa kutosha wa kulala ni njia moja wapo inayopendekezwa na wataalamu katika kupunguza machungu ya hangover. Mara nyingi mtu anapokuwa amekunywa sana, kulala kwake kunakuwa ni kwa taabu, anaweza akalala mwanzoni lakini baada ya muda usingizi huweza kumuishia na au kuanza kushituka mara kwa mara. Kwahiyo kama siku itakayofuata utapata muda wa kulala na ukalala "mwili wako unaweza ukakushukuru"

Hitimisho.

Kuna njia nyingine nyingi zaidi ya hizi nilizotaja ambazo zinaweza kutmiwa na watu katika kuwaondolea maumivu ya hangover. Cha muhimu ni kuchagua njia sahihi na kufuata ushauri wa kitaalamu kwani njia nyingine zikausababishia mwili madhara kiafya.

"Bao la mkono" la Nape latua Tume ya Uchaguzi

Dar es Salaam. Kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye bado inawaumiza vichwa wapinzani nchini baada ya viongozi hao jana kuitamkia wazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuwa hakuna haja ya kujadili maadili wakati CCM tayari kimesema ‘kitafunga bao la mkono.’
Wakizungumza kwenye mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya Uchaguzi jana, baadhi ya viongozi hao walitaka mkutano huo usitishwe hadi pale CCM itakapomuonya Nape.
Wa kwanza kuibua mada kuhusu Nape, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi ambaye alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo hadi NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa na IGP wakemee kauli hiyo.
“Hivi tutayazungumziaje maadili, mbona CCM kimeshaonyesha kuwa hakitafuata maadili, kuna haja gani ya kuzungumzia wakati wameshasema watafunga hata kwa goli la mkono?” alisema Dk Makaidi.
Awali akiwa katika ziara ya Kinana wilayani ya Sengerema, Nape alikaririwa akisema kuwa ana uhakika CCM itashinda baada ya kuona mwitikio mkubwa wa Watanzania katika ziara hizo.
“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” alisema Nape.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva aliwatoa wasiwasi wanasiasa hao akiwaambia kuwa Nec itafanya uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na hivyo kauli ya Nape haiwahusu.
“Maadili tunayoyatengeneza yataanza kutumika kuanzia Agosti 22, wakati wa kampeni, lakini iwapo kuna vurugu zinatokea baina ya vyama sisi wala Nec hatuhusiki,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa akichangia kipengele cha wahusika wa maadili aliitaka Nec kuliweka Jeshi la Polisi kupitia IGP kusaini na kuwa mhusika katika masuala ya maadili ya uchaguzi.
Hiki kipengele cha 1.3 kinawataja wahusika wa maadili kuwa ni vyama vya siasa, wagombea, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Nec pekee.
“Kutokana na uzoefu tulionao katka chaguzi zilizopita, Jeshi la polisi ni washiriki wakubwa katika masuala ya uchaguzi, kama jeshi hilo halitasaini maadili hayo basi kutakuwa na matatizo makubwa katika uchaguzi huo,” alisema.
Awali akifungua mkutano huo Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kufuata maadili, sheria na kanuni za uchaguzi, na katika kipindi chote cha kuanza kwa kampeni hadi siku ya uchaguzi.
Alisema kila chama na mgombea kitatakiwa kuheshimu na kutekeleza kanuni na sheria za uchaguzi, siku moja baada ya uteuzi wa mgombea ili kuepesha vurugu zinazotokea kipindi cha uchaguzi.
“Maadili tutakayojadili leo (jana), yatahusisha mambo mbalimbali yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa na wagombea wao kipindi cha kampeni hadi uchaguzi,” alisema Jaji Lubuva na kuongeza kuwa;
“Mfano kwa vurugu za aina yoyote katika mkutano wa chama kingine cha saiasa, sanjari na maadili yanatakiwa kufuatwa wakati wa upigaji kura hadi kutangazwa kwa matokeo.
Souce: Mwananchi

HUKUMU YA KESI YA BASIL MRAMBA NA WENZAKE KUTOLEWAJUMATATU


Hukumu ya kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 inayomkabili Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na wenzake imeahirishwa kwa mara ya pili kwa sababu hakimu anaumwa.
  
Kesi hiyo ilitajwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomwa kwa hukumu, baada ya kuahirishwa kwa mara ya kwanza Mei 30 mwaka huu.
  
Hata hivyo, Hakimu Mkazi, Saul Kinemela alisema hawezi kusoma hukumu hiyo kwa sababu Mwenyekiti anayeunda jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, John Utamwa, hajafika mahakamani kwa kuwa anaumwa na amepewa siku mbili za mapumziko.
  
Hakimu Kinemela aliahirisha hukumu hiyo hadi Jumatatu ya Julai 6, mwaka huu. Hakimu mwingine katika jopo hilo ni Sam Rumanyika.
  
Mbali na Mramba washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

Wabunge 11 Wa UKAWA Watimuliwa Bungeni Kisa Kupinga Muswada wa Sheria ya Petrol


Dodoma: Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Watanzania limewasimamisha wabunge 11 kwa kudharau mamlaka ya Spika jana.
  
Hatua hiyo ni baada Spika wa Bunge hilo, Anne Makinda, kuwashitaki katika Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, wabunge hao wa Kambi Rasmi ya Upinzani, wakiongozwa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).
Makinda alichukua hatua hiyo, baada ya wabunge hao kurudia kwa mara ya pili kufanya vurugu na kupiga kelele wakati kikao kikiendelea na kumlazimisha kuahirisha kwa mara ya nyingine shughuli za bunge zilizokuwa zikiendelea bungeni mjini hapa.
“Bunge haliwezi kuendeshwa kwa kelele na vurugu namna hii. Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, ninawataja kwa majina vinara wa vurugu ambao walitakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili na kulazimika kuahirisha Bunge hilo hadi jioni."
Hukumu ya Watuhumiwa
Kamati hiyo ilitoa adhabu kwa mafungu matatu ambapo wapo ambao hawakutoa ushirikiano kabisa kwa kamati hiyo wakidai wangefanywa hivyo mbele ya wanasheria wao, hao walifungiwa moja kwa moja, waliotoa ushirikiano kwa kamati wakafungiwa kutohudhuria vikao viwili na wengine waliochelewa kupata wito wanatakiwa kuhojiwa na kama leo asubuhi saa nne wakati mmoja hakuguswa na adhabu hizo kabisa.
Waliosimamishwa moja kwa moja ni Lissu, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekul (Chadema), Mbunge wa Mohambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi) na Mbunge wa Kasulu Mjini na Moses Machali (NCCR-Mageuzi).
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema), Rashid Ally Abdallah (CUF) na Mbunge wa Gando, Khalifa Khalifa (CUF), hao wanatakiwa kufika katika kamati hiyo ya maadili leo kwa kuwa hawakupata wito wa kuitwa jana mapema huku Mbunge David Silinde hakuguswa kabisa katika adhabu hiyo.
Kundi la pili waliofungiwa vikao viwili, cha leo na Jumatatu ni Mbunge wa Ole, Rajab Mbaruk Mohamed (CUF) na Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) ambao waliitikia wito na walitoa ushirikiano kwa Kamati hiyo ambayo Makamu Mwenyekiti wake ni Brigedia Hassan Ngwilizi, ambaye ni Mbunge wa Mlalo (CCM).
Akiwasilisha maamuzi ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati alisema walifikia maamuzi hayo baada ya kuridhika baada ya kuwaita wahusika na kujieleza na hatimaye kufikia maamuzi hayo.
Kamati hiyo ambayo Makamu Mwenyekiti wake ni Kapteni John Chiligati, ambaye ni Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM) ilitoa maamuzi hayo kulingana kanuni za Bunge.
Ilivyokuwa
Vurugu hizo zilianza mara baada ya Lissu kusimama kuomba Mwongozo wa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipokuwa akisoma kwa mara ya pili, muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesi wa mwaka 2015, ambao Kambi ya Upinzani ilikuwa ikiupinga tangu mwanzo.
Wakati wakipiga kelele, Spika alinyamaza na Simbachawene akaendelea kusoma muswada huo, ndipo wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani wote waliokuwepo bungeni wakasimama kumuunga mkono Lissu na kuwalazimu baadhi ya wabunge wa CCM kuanza kuwazomea na wao kurudisha maneno yaliyosababisha hata aliyekuwa akisoma asisikike.
Msimamo wa upinzani
Pamoja na yaliyotokea, kambi hiyo ilijikusanya ndani ya Bunge hilo kupeana misimamo ambapo, walisikika wakisema hata iweje, hawatakubali muswada huo wa Sheria ya Mafuta na Gesi upite.
Katika hatua nyingine, Spika Makinda alikataa kuendekeza malalamiko ya Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlata (CCM), aliyeomba mwongozo na kudai kuwa, Mbunge wa NCCRMageuzi, Moses Machali alimdhalilisha kwa kumwambia kuwa, alifumaniwa na wajinga wenzake.
Machali alisema hivyo alipokuwa akitoa maoni ya muswada uliopitishwa wa Ulinzi wa Mtoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi, baada ya kukasirishwa na kitendo cha Mlata kuropoka kuwa Mbunge huyo aliyetaka adhabu iwe kunyongwa ni kichaa.
“Leo wote mmeonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu, kwa kutoleana maneno yasiyofaa. Wengine mmekuwa mkiingilia hoja za wenzenu wakati wanaziwasilisha, kwa kuwatolea maneno yasiyo na adabu,” alisema.

ACT yailalamikia CHADEMA kuhujumu mikutano yake.


CHAMA cha Alliance for Change and Transparency(ACT), kimebaini kuwepo kwa mipango inayoratibiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuhusika kuhujumu mikutano yake mbalimbali.
Hujuma hizo zimebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Mipango na Mikakati Taifa  wa ACT Habibu Mchange, aliyesema kuwa chama hicho kimekuwa kikihangaikia ACT na kusahau kushughulikia matatizo ya watanzania.
“Chadema wamekuwa wakitufuatilia kila mahali tunapofanya mkutano na hilo wamekuwa wakifanya kwa sababu ya kutuhofia. Kwa mfano tulipokuwa na mkutano Mwanza na wao wakatangaza kufanya tukawashinda, kesho tumetangaza kufanya mkutano na wao wametangaza kufanya Kawe.
“Chadema tunawaonea huruma kwa kuwa tutawafanya kitu ambacho hawatasahau katika historia ya siasa za tanzania kwa sababu njia nyingi wanazotumia ni zile tulizoziratibu wakati tukiwa huko,”alisema Mchange.
Katika hatua nyingine Mchage alisema baada mbalimbali mikoani hivi sasa ACT kupitia viongozi wake  wa kitaifa wameandaa kufanya mkutano mkubwa kesho jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwembe Yanga.
“Mkutano huo utatoa fursa ya kuzindua Ilani ya jiji la Dar es salaam, itakayotokana na ilani Kuu  ya chama ili kukabiliana na kero mbalimbali za jiji.
“mkutano huo utatoa fursa ya ACT kuwataka watanzania kuishi katika misingi ya haki, undugu, umoja na mshikamano kwa kutumia azimio la Tabora lilozinduliwa na chama hicho likiwa limewisha azimio la Arusha,”alisema.
Chama hicho kinatarajia kusimamisha madiwani, wabunge na nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akizungumzia tuhuma hizo msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alisema chama hicho hakina muda wa kuzungumzia tuhuma ambazo hazina mashiko.

Friday, July 3, 2015

Wanne hawakurejesha fomu za CCM kuwania Urais Tanzania 2015

 
Watu wanne waliochukua fomu za kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wagombea wa kiti cha urais wametoka rasmi katika mchakato huo, baada ya kushindwa kurudisha fomu hadi muda wa mwisho ulipofika saa 10.00 alasiri ya jana.
Watu hao ni 
  1. Peter Nyalali
  2. Helen Elinewinga
  3. Anthony Chalamila
  4. Dk Muzamil Kalokola
Jumla ya wanachama 42 walijitokeza kuchukua fomu hizo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi alisema zoezi la kuchukua fomu lilianza Juni 3, mwaka huu na lilitarajia kumalizika Julai 2, 2015.
“Mmoja wa wachukua fomu, Helena Elinawinga alitelekeza fomu hizo kwa mmoja wa maofisa wa CCM baada ya kufika kuomba ushauri huku akitaka kupewa kwanza elimu ya siasa kabla ya kuanza kutafuta wadhamini” 
Luhwavi alisema hatua itakayofuata ni mchakato wa vikao vya chama kuanzia Jumanne wiki ijayo.