Na. Mtaalamu wetu:
KWA UFUPI
"Wataalamu wanaamini kwamba kuongezeka kwa uelewa kuna weza saidia kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo"
Uchunguzi wa hivi karibuni unaonyesha kwamba katika nchi zilizoendelea kama Marekani asilimia 50 ya vifo yanatokana na magonjwa ya moyo na matatizo katika mishipa ya damu, hasa kwa watu wazima wenye umri kati ya miaka 45-79. Visababishi vikubwa vimekua ni vile Uvutaji wa sigara na Unene kupita kiasi .
Ingawa idadi yavifo imepungua kwa miaka thelathini iliyopita kutokana na matibabu, magonjwa ya moyo katika nchi ya Marekani bado yanaongoza katika kusababisha vifo.
Hali hii ya magonjwa ya moyo imeanza kuzinyemelea na kuwa tatizo katika nchi zinazoendelea kwa kasi kutokana na kubadilika kwa mifumo na hali ya maisha au kwa kitaalamu wanasema "Life style".
Wakati wenzetu wanchi zilizoendelea wanajitahidi kujirudi na kuishi maisha ya kawaida, hali imekua ni tofauti katika nchi za kiafrika.
Wakati wenzetu wanchi zilizoendelea wanajitahidi kujirudi na kuishi maisha ya kawaida, hali imekua ni tofauti katika nchi za kiafrika.
Kwamujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO); robo tatu ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu vinatokea kwenye nchi zinazoendelea. Katika vifo milioni kumi na sita vinavyotokea kwa wenye umri wa miaka 70 kwa sababu ya magonjwa yasiyoambukiza, 82% vinatokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, na katiya vifo hivyo 37% ya vifo vinatokana na magonjwa ya moyo na matatizo katika mishipa ya damu.
Visababishi ni nini?
Sababu kubwa inayosababisha matatizo ya magonjwa ya moyo ni tabia hatarishi au kwa lugha ya kigeni "behavioural risk factors ". Moja kati ya tabia hizo hatarishi ni kutokufuata utaratibu katika ulaji wa vyakula hasa kwa kupendelea zaidi vyakula vya kukaanga "fast food" na vyenye chumvi na sukari nyingi, kutokufanya mazoezi au kufanya mazoezi bila kufuata ushauri wa kitaalamu , matumizi ya sigara na matumizi makubwa ya vilevi.
Tabia hatarishi husababisha kupanda kwa presha ya damu, kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu, kuongezeka kwa mafuta katika damu, kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi "obesity".
Nini cha kufanya?
Vitu vya muhimu vya kufanya ili kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo na katika mishipa ya damu ni kupunguza matumizi ya sigara, kupunguza matumizi ya chumvi katika vyakula, kuongeza ulaji wa matunda na mbogamboga badala ya nyama nyekundu, kufanya mazoezi na kupunguza matumizi ya vileo.
Vile vile matibabu ya magonjwa kama vile kisukari, na shinikizo la damu husaidia kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo na mishipa ya damu.
Hitimisho
"Study" zinaonyesha kwamba kuongezeka kwa uelewa wa masuala ya afya kunasaidia kupunguza ukubwa wa tatizo na uchunguzi unaonyesha kwamba matatizo haya yanawakumba zaidi watu ambao wana uelewa mdogo au ambao hawana uelewa kabisa.
Kwakuwa umeshapata uelewa ni matuaini yangu utabadilisha tabia zako hatarishi.
No comments :
Post a Comment