WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa amepata
udhamini wa kishindo katika mkutano uliofanyika jana katika ofisi kuu ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
Lowassa alipata udhamini huo baada ya wanachama
kujitokeza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni,
Dar, ambapo alipata zaidi ya wadhamini 212,150 huku akisema Dar imevunja
rekodi ya mikoa yote ya Tanzania.
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika
mkutano huo Lowassa alisema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini
kwa kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa moyo na maneno ya watu yanayovumishwa
kuwa anawapatia fedha ili wafike kwenye mkutano wake .
Lowassa aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe
ridhaa ya kuwa rais wao kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji
mbovu wa kusuasua anausimamia kwa haki na weredi na ndani ya miezi sita tayari
matokeo yatakuwa yameonekana.
“Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu
yaani nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze
maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua,” alisema.
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale
Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa
Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea
huyo.
Zoezi hili lilifanyika jana jioni ya Juni 27, 2015
kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar ambapo Lowassa
alipata jumla ya Wadhamni 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa
kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini
No comments :
Post a Comment