Monday, July 27, 2015

HAMA HAMA ZA WABUNGE, ZAMKUMBA LETICIA NYERERE

Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi wa habari

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi
nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).



Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.



Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.

“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia”

amesema Leticia.


Leticia amesema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.



Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi. 





Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam

No comments :

Post a Comment