Friday, July 3, 2015

Wanne hawakurejesha fomu za CCM kuwania Urais Tanzania 2015

 
Watu wanne waliochukua fomu za kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wagombea wa kiti cha urais wametoka rasmi katika mchakato huo, baada ya kushindwa kurudisha fomu hadi muda wa mwisho ulipofika saa 10.00 alasiri ya jana.
Watu hao ni 
  1. Peter Nyalali
  2. Helen Elinewinga
  3. Anthony Chalamila
  4. Dk Muzamil Kalokola
Jumla ya wanachama 42 walijitokeza kuchukua fomu hizo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi alisema zoezi la kuchukua fomu lilianza Juni 3, mwaka huu na lilitarajia kumalizika Julai 2, 2015.
“Mmoja wa wachukua fomu, Helena Elinawinga alitelekeza fomu hizo kwa mmoja wa maofisa wa CCM baada ya kufika kuomba ushauri huku akitaka kupewa kwanza elimu ya siasa kabla ya kuanza kutafuta wadhamini” 
Luhwavi alisema hatua itakayofuata ni mchakato wa vikao vya chama kuanzia Jumanne wiki ijayo.

 

Bunge Laahirishwa Ghafla Tena leo, baada ya Wapinzani kugomea Muswada wa Mafuta na Gesi Asilia

 
 
Dodoma: Waziri wa Nishati na madini George Simbachawene alipoanza kusoma kwa mara ya pili Muswada wa mafuta na gesi asilia (Muswada juu ya Petroli, 2015 The Petroleum Act, 2015), Tundu Lissu alisimama na kuomba Kuhusu utaratibu, Spika hakumpa nafasi, ndipo wabunge wote wa UKAWA Waliposimama na kuanza kupiga kelele wakisema Muongozo muongozo..!!.

Spika Kamuomba Waziri aliyekuwa anasoma Hotuba akakae kisha akawataja baadhi ya wabunge kwamba ndio wanaoleta fujo bungeni kwa kosa kutokana na kanuni ya kuleta fujo bungeni ambao ni:

1.John Mnyika Mbunge wa CHADEMA jimbo la Ubungo

2.Tundu Lissu Mbunge wa CHADEMA jimbo la Singida Mashariki

3.Ernest Silinde Mbunge wa CHAEMA jimbo la Mbozi Magharibi

4.Rashid Ali Abdalla mbunge wa CUF jimbo la Tumbe Zanzibar

5.Paulina Gekul Mbunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA wa Mkoa wa Manyara

6.Moses Joseph Machali Mbunge wa NCCR-Mageuzi Jimbo la Kasulu Mjini

7.Rajab Mbarouk Mbunge wa CUF Jimbo la Ole Zanzibar

8.Felix Francis Mkosamali Mbunge wa NCCR Mageuzi jimbo la Muhambwe

9.Rev. Simon Peter Msigwa Mbunge wa CHADEMA jimbo la Iringa Mjini

10.Joseph Roman Selasini Mbunge wa CHADEMA jimbo la Rombo

11.Khalifa Suleiman Khalifa Mbunge wa CUF Jimbo la Gando Zanzibar

Bunge limesitishwa hadi watakapoitwa tena na Spika, vilevile kamati ya Maadili imeitwa kujadili hili Swala.


 

UNAFAHAMU KWAMBA MTU ANAWEZA KUWA "ADDICTED" NA MISOSI?

                       

Na. Mchambuzi wetu

Utangulizi

Suala la mtu kuwa "addicted" na chakula ni suala jipya ambalo wana-science wanaliangalia kwa ukaribu. Majaribio mengi yaliyofanyika kwa wanyama na binadamu yanaonyesha kwamba, kwa baadhi ya watu sehemu ambayo inakua "affected" au inayo-athiriwa na madawa kama vile cocaine na heroin vile vile hu dhiriwa na vyakula, ususani vyakula ambavyo ni vitamu. Vyakula ambavyo ni vitamu mara nyingi hutengenezwa kwa viambata vya sukari, chumvi na mafuta.
"Wapenda chipsi mpo?"

Kama yalivyo madawa ya kulevya, vyakula ambavyo ni vitamu sana husisimua kutengenezwa kwa kemikali iyoratibu kujisikia furaha au amani inayoitwa "dopamine"
.
Iwapo kemikali hii itatengenezwa na kumfanya mtu ajisikia vizuri, mtu huyo ataendelea kukipenda hicho chakula. Vilevile, chemikali hiyo itamfanya huyo mtu atake kukitumia chakula hicho mara kwa mara. Kitendo hichi kwa kitaalamu kinaitwa "reward pathway".

"Reward pathway" huweza kukua na kuzidi mifumo au "pathways" zingine inazohusiana na kutosheka nakushiba na hivyo kumfanya mtu awe anakula muda wote bila ya kushiba wala kutosheka hata kama hana njaa.

Watu wenye tatizo hili wanaweza kula mara kwa mara na jinsi wanavyokula ndivyo hamu ya kula inapozidi.

Wanasayansi wanaamini kwamba "food addiction" ndiyo sababu kubwa ya watu kupata unene uliozidi "obesity" ingawa hali hii huwapata ata  watu ambao wanamaumbo ya kawaida .

 Watu wenye "addiction" ya chakula huendelea kula kwa wingi ingawa hupata  madhara kama vile kuongezeka kwa uzito na matatizo katika mahusiano.

Kama ilivyo kwa watu waliokuwa "addicted" madawa ya kulevya, watu waliokuwa addicted kwenye vyakula hupata wakati mgumu katika kuacha hiyo tabia ata kama watajaribu.

Dalili za mtu mwenye addiction ya chakula.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Yale " Yale University's Rudd Center for Food Science & Policy walitengeneza "questionnaire" ili kuweza kuwabaini watu wenye tatizo la "Food Addiction" au kwa Kiswahili "Arosto ya Chakula"(Declaimer: Utanijulisha kama nimekosea jina"). Ili uweze kujipima maswali hayo utayapata HAPA.
have developed a questionnaire to identify people with food addictions. 

Unawezaje kumsaidia mtu mwenye " addiction" ya chakula?

Wanasayansi bado wanafanya kazi ili kuweza kuelwa kwa undani kiini cha "addiction" ya chakula. Wengi wanatoa maoni kwamba kupona addiction ya chakula itakua ni vigumu kuliko kupona addiction ya vileo.
"SIJUI WEWE UNAMAONI GANI"

 

Upinzani ‘walianzisha’ tena bungeni


 
Dodoma. Mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika jana ulizua kizaazaa na kumlazimisha Spika Anne Makinda kuahirisha kikao baada ya kukosekana utulivu ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Kikao hicho kiliahirishwa muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu wakati Bunge lilipotakiwa kukaa kama kamati kumalizia kiporo cha Muswada wa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi wa mwaka 2015 ambao mchakato wa kuupitisha haukukamilika juzi kutokana na muda kuisha.
Ilikuwa ni kama marudio ya hali ilivyokuwa mwishoni mwa mwaka jana wakati wabunge wa upinzani waliposimama na kuweka mazingira ambayo yalizuia shughuli za chombo hicho kuendelea wakati wa kujadili sakata la escrow.
Pages: 2 3

MAPENZI: AMUUA MWENZAKE KWA KISU WAKIGOMBEA MWANAMKE


WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.

Waliokufa ni Chacha Mwita (24) aliyechomwa kisu kifuani na mwenzake wakigombea mwanamke wa baa huko Sirari. 


Wengine ni Juma Nguka (25) aliyeuawa na watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kupora pikipiki yenye namba za usajili MC 936 ACA, mali ya Erick Jumanne mkazi wa Kijiji cha Mkoma.


Tukio lingine ni kufa maji kwa mvuvi aliyefahamika kwa jina la Wambura Maregeri (30) mkazi wa kijiji cha Muhundwe aliyekufa maji baada ya Boya kutoboka.


Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP Swetbert Njewike alisema kuwa matukio hayo matatu ya vifo yalitokea Julai mosi mwaka huu katika Wilaya za Rorya na Tarime.


Akielezea tukio la baa ambalo Mwita aliuawa, alisema siku hiyo marehemu akiwa baa moja katika mji wa Sirari, Tarime, nyakati za saa moja jioni kulitokea ugomvi kati ya marehemu na mtu mwingine ambaye hajafahamika jina lake wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina.


Alisema wakati wa ugomvi huo, Mwita alichomwa kisu kifuani na aliyefanya kitendo hicho alitoroka ambapo majeruhi huyo alitokwa damu nyingi na alipofikishwa Hospitali ya Wilaya Tarime alifariki dunia.


Alisema Nguka yeye alipoteza maisha baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kudaiwa kuiba pikipiki. 
 
Akasema Maregesi alikufa maji baada ya boya lililotengenezwa kienyeji alilokuwa anatumia katika uvuvi kutoboka na kuzama majini hali iliyopelekea kifo chake.


“Jeshi la Polisi linafanya msako wa watuhumiwa wa mauaji Chacha Mwita na watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya Nguka ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria,” alisema.


Aliwaonya wananchi kutojichukulia sheria mikononi ya kuwauawa watu wengine badala yake wawafikishe katika vyombo husika vikiwemo vya Dola. 
 
 Aliwaomba raia wema kutoa taarifa mara watakapowaona watuhumiwa hao wa mauaji hayo ii wakamatwe.

SHINYANGA: Polisi yakamata mashine ya BVR kwa kiongozi wa CHADEMA

Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wa Nyakato wilayani humo Mayunga Alphonce (CHEDEMA), huku wakiwalipa shilingi 5,000/= kila mmoja.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika mtaa wa Nyakato ambapo mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura.

Mpesya amesema kuwa vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.

Ameongeza katika harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo.

Mpesya amesema jeshi la Polisi wilayani humo linamshikilia Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyasubi, Lugina Misango ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Katika hatua nyingine, Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo, kutambua kuwa ofisi yake ina mamlaka kamili ya serikali na kwamba wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo upo katika kituo cha polisi.

Source: Habari hii nimeinukuu kutoka Malunde 1 Blog

KESI YA GWAJIMA YAPIGWA KALENDA

Dar es salaam: MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana imeshindwa kumsomea maelezo ya awali Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya matusi na kushindwa kuhifadhi silaha.
Kesi hiyo ilitajwa jana kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali lakini iliahirishwa kwa kuwa Hakimu Mkazi Wilfred Dyansobera anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo mahakamani.
Hakimu Mkazi, Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hiyo Julai 20, mwaka huu kwa ajili ya washitakiwa hao kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Dyansobera.
Mbali na Gwajima washitakiwa wengine, ni Mlinzi wake, George Mzava, Msaidizi wake, Yekonia Bihagaze (39) na Mchungaji Georgey Milulu (31) wanakabiliwa na shitaka la kukutwa na silaha pamoja na risasi kinyume cha sheria.
 Katika kesi ya kwanza namba 85, Gwajima anadaiwa kati ya Machi16 na 25, mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam alitoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akimueleza Askofu kwamba ni mtoto, mpuuzi asiye na akili katika namna ya kwamba ingeleta uvunjifu wa amani. 
Katika kesi nyingine namba 84 , Gwajima anakabiliwa na mashitaka ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi wa silaha za moto. 
Anadaiwa kati ya Machi 27 na 29, mwaka huu, ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam, alishindwa kuhifadhi silaha aina ya Beretta namba CAT 5802, risasi 3 za pisto na risasi 17 za shotgun. 

Katika mashitaka mengine yanayowakabili washitakiwa wengine, inadaiwa Machi 29, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ Mikocheni ‘A’ walikutwa wakimiliki silaha na risasi hizo bila ruhusa kutoka mamlaka husika