Saturday, June 27, 2015

Dk Shein, Maalim Seif wapishana kauli waliosusia Baraza la Wawakilishi

Tokeo la picha la dr. sheinZanzibar/Dar. Wakati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, ameunga mkono kitendo cha mawaziri na wajumbe wa CUF kususia baraza, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amekipinga.

Kauli tofauti za viongozi hao wa ngazi ya juu katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), zimekuja baada ya mawaziri na wawakilishi wa CUF kutoka ndani ya Baraza la Wawakilishi, wakisusia kujadili muswada wa Sheria wa Bajeti Kuu ya matumizi ya Serikali ya mwaka wa fedha 2015/2016.

Akizungumza na Mwananchi jana, Maalim Seif alisema wajumbe waliona njia sahihi ya kufanya ni kutoka ndani ya baraza, kwa sababu walikuwa hawasikilizwi kila wanapozungumzia mchakato unaoendelea kwa sasa wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura.

Maalim alisema anashangazwa na wajumbe wa baraza kushindwa kujadili hoja iliyojitokeza, kiasi cha kusababisha baadhi ya wajumbe kususia kikao cha bajeti.

Alisema alisema kwamba tangu kuanza kwa uandikishaji, kumekuwa na mambo yanayofanyika kinyume kabisa na sheria, yakiwamo watoto chini ya umri wa miaka 18 kuandikishwa katika daftari la wapiga kura, vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kutisha watu huku wakiwa wamevaa ‘kininja’, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

“Ni wazi inaonyesha kwamba kuna kasoro kwenye uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu na usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar mkazi,” alisema.

Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, SUK, Maalim Seif alisema kwamba haiwezi kuvunjika, kwa sababu hakuna wa kuivunja kwa kuwa ilipitishwa kwenye Azimio la Baraza la Wawakilishi.

Hivyo, ikiwa inatakiwa kuvunjwa ni lazima, Serikali ifuate sheria ya kuanza mchakato wa Kura za Maoni, kuuliza wananchi watoe maoni yao na kisha kufikisha tena kwenye Baraza la Wawakilishi waijadili.

Pia alisema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea kwa SUK, wanastahili kujiuzulu au kufukuzwa ndani ya vyama vyao.

Alisema kuwa, hoja ya CCM kutaka kufuta SUK inapaswa kulaaniwa kwani italeta machafuko Zanzibar.

“Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM wala CUF tu, ni ya wananchi wote, ni makosa makubwa kudhani kuwa Serikali hiyo ni ya vyama hivyo viwili. Ilifanyika hivyo ili kutokuendelea umwagaji damu,” alisema.

“Tangu asubuhi kwa hapa Zanzibar ilifahamika kabisa kwamba nitazuiwa kuingia kwenye kikao cha Baraza la Wawakilishi hata watoto walijua ‘’alisema.
Source: Mwananchi

Mwandosya amuita Lowassa kambi yake

Dodoma. Profesa Mark Mwandosya, ambaye anawania kuteuliwa na CCM kugombea urais, amemtaka Edward Lowassa kujiunga na kambi yake kwa kuwa makada wengine wanne kwenye mbio hizo wanamuunga mkono.
Hata hivyo, wawili kati ya makada hao wanne wamekana kumuunga mkono.
Mwandosya, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), alisema tayari Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Steven Wasira, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wanamuunga mkono na hivyo kumshauri Lowassa kujiunga na kambi yake.
“Kama (wagombea) wengi wananiunga mkono, aliyebakia basi atakuwa ni ndugu yangu, rafiki yangu, Edward Lowassa. Naye angesema hivyo ingerahisisha sana kazi ya chama, ingepunguza sana kazi, makundi yangekuwa yameisha,” alisema Mwandosya baada ya kurejesha fomu za kuomba CCM impitishe kugombea urais.
“Halmashauri Kuu isingepata shida, Kamati Kuu isingepata shida nadhani tungeweza kufika pale ambako tungefika tarehe 12 (Julai, siku ambayo Mkutano Mkuu wa CCM utamchagua mgombea urais), bila kikwazo, bila makundi,”alisema mbunge huyo wa Rungwe Mashariki jana.
Lakini kauli yake imepokewa kwa hisia tofauti na watu hao aliodai wanamuunga mkono, huku kambi ya Lowassa ikizungumzia kauli hiyo kuwa si ya mtu aliye makini kwenye mbio za urais.
Jumla ya makada 40 wamechukua fomu za kuomba ridhaa ya CCM kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25 na chama hicho kina kazi ngumu ya kumpata mwanachama atakayemrithi Rais wa sasa, Jakaya Kikwete ambaye katiba inamzuia kuendelee kuongoza baada ya kumaliza vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja.
Mgombea urais wa CCM pia ndio atakuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza mara baada ya kurudisha fomu jana, Profesa Mwandosya alisema mchakato huo umewafanya wanaoomba urais kuwa marafiki zaidi licha ya kupigana vijembe, akisema ingekuwa nchi nyingine wangefanyiana vurugu.
Aliwashukuru wagombea wenzake waliotamka hadharani kuwa watamuunga mkono endapo hawatapitishwa na Kamati Kuu ya CCM kugombea urais.
“Namshukuru Benard Membe ambaye  ametangaza na kuandikwa (kwenye vyombo vya habari) kwamba yeye ameona katika orodha yote ya watu 40, kama si yeye basi ataniunga mkono mimi na yupo tayari kuzunguka nchi nzima iwapo chama kitaniteua kuwa mgombea,” alisema Profesa Mwandosya.
“Namshukuru pia Mheshimiwa Pinda, amelizungumzia hili katika vituo kama si kimoja viwili kuwa moyo wake utakuwa na furaha kama Profesa Mwandosya anaweza kuteuliwa na chama.”
Source: Mwananchi

Morogoro: Watu watatu wafariki katika mapambano na Polisi, wawili wanasadikiwa kuwa Al Shabaab..Wengine 50 wanasakwa

Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabaab katika mapigano baina yao na jeshi la Polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu hao walikuwa wamejificha msituni.

Amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi unafanyika ikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo.

Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ya Turian mkoani Morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo ambapo kati ya hizo,maiti mbili zinaonekana kuwa ni za watu wasio raia wa Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu ambaye alijeruhiwa vibaya na badaye kufariki akiwa hospitalini hapo.
 
NEC yaahirisha uandikishaji kwa BVR Dar es salaam na Pwani

Kuahilishwa kwa zoezi la Uboreshaji kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuahirishwa kwa tarehe ya kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani hadi hapo itakapotangazwa tena.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Tume hiyo na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwana Julius B. Mallaba leo imesema hatua hiyo imetokana na kuchelewa kuwasili kwa vifaa vya kuandikishia Wapiga Kura (BVR), ambavyo viko katika Mikoa ambayo zoezi la Uboreshaji linaendelea.
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa Tume imelazimika kupeleka vifaa vilivyotarajiwa kutumika katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani , kwenda katika mikoa iliyoonyesha kuwa na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hali inayotafsiriwa kuwa ni kuongezeka kwa mwamko miongoni mwa wananchi wanaojitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Awali Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya “Biometric Voters Registration” (BVR) kwa Mkoa wa Pwani ulipangwa kuanza tarehe 25/06/2015, Aidha kwa Mkoa wa Dar es salaam Uandikishaji ulitegemewa kuanza tarehe 04/07/2015.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa rai kwa wananchi wa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam kuwa watulivu wakati ambapo ikisubiri vifaa vya Uandikishaji kutoka katika Mikoa itakayokuwa imekamilisha zoezi hilo.

Tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2014

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014
ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Majina pia yapo kwenye tovuti ya TAMISEMI www.pmoralg.go.tz na Ofisi ya Kamanda wa Polisi
wa Mkoa/Wilaya iliyo karibu nawe ukatazame endapo jina lako ni miongoni mwa walioitwa
kwenye usaili.
Usaili utafanyika katika miji ya makao makuu ya mikoa Tanzania Bara Kwa tarehe
zilizooneshwa kwenye jedwali kwenye link hapo chini
Ni vema ukachungulia shule za katani kwako ili ukimwona mhusika apewe taarifa ili akashiriki.
Usaili utaanza 03.07.2015

Mahakama Kuu Dar yatoa uamuzi kuhusu ishu ya Chenge na ESCROW

Tokeo la picha la CHENGE
Ishu ya ESCROW ni kama kuna watu wengi walianza kuisahau hivi. Jana  imerudi  tena   kwenye masikio ya watu ambapo tunakumbuka kuna orodha ya Mawaziri na Wenyeviti wa Kamati za Bunge walisimamishwa baada ya kutajwa kuhusika na mgao wa Bil. 300 zilizokuwa kwenye account ya ESCROW.
 
Mbunge Andrew Chenge alikuwa mmoja ya waliotajwa kuhusika pia, ishu ikapelekwa Kamati ya Maadili na baadae Mbunge huyo akapeleka ombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ili kuzuia kuhojiwa na Kamati hiyo.
 
Jana June 26 2015 ripoti kutoka Mahakamani inasema Mahakama hiyo imetupilia mbali Ombi hilo kwa kuwa imeona haikuwa na Mamlaka ya kuzuia Shauri hilo, na walichokiona ni kwamba Chenge alikuwa na njia mbadala kushughulika na ishu hiyo badala ya kukimbilia Mahakamani
 
SAKATA LA FAIZA ALLY LATUA BUNGENI

Siku chache zimepita tangu hukumu ya kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kutolewa dhidi ya mzazi mwenzake Faiza Ally,baada ya kuiomba mahakama kumchukua mtoto wao, hali iiyopelekea mahakama kutoa hukumu kuwa mtoto achukuliwe na Mbunge huyo,  jambo lililofanya sakata hilo kutinga bungeni.
 
Baadhi ya wabunge na wadau mbalimbali wamedai kuwa mtoto bado ni mdogo sana kuweza kuishi na baba yake na kutoa maoni kuwa mtoto arudishwe kwa mama yake kwa kuwa kila mtu ana mapungufu na kusema kuwa mtoto bado ana haki ya kuwa karibu na mama yake.
 Kwa mujibu wa Mbunge Martha Mlata jana  alisema kuwa; “Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake”.
Hoja hiyo ikachangiwa na Mbunge David Kafulila alisema “Hii nchi ina mihimili mitatu, Bunge, Mahakama na Serikali… Tuheshimu maamuzi ya Mahakama”.
 
Tokeo la picha la FAIZA ALLY KILIMANJAROTokeo la picha la FAIZA ALLY KILIMANJARO
 Sambamba na hilo Waziri Saada Mkuya akahitimisha na kusema; “Kama mama na mimi nilipoisikia ile taarifa nilipata uchungu, kila binadamu ana mapungufu yake lakini mtoto alelewe na mama yake”.

UMUHIMU WA NYWELE KICHWANI

Na mchambuzi wetu.

 Mitindo ya nywele ni kati ya vitu vinavyotumika katika kumfanya mtu awe na muonekano mzuri na urembo. Wakati mwingine mitindo ya nywele huhusianishwa na utamaduni kama vile "Masai Style" au umarufu nafikiri unaifahamu "Baloteli style" .

 Maranyingi mitindo ya nywele hubadilishwa ili kumpa mtu muonekano mpya au kumfanya mtu aonekane wa kisasa zaidi kwa wakati huo. Nadhani unafahamu vizuri kuhusu mitindo ya nywele inayokua maarufu kipindi Fulani na kupotea.
 Niwangapi mnafahamu kwamba nywele ni Chanzo kikubwa cha Nguvu kwa binadamu? Nikiongelea nguvu namanisha nguvu za kila aina kuanzia misuli yetu hadi nguvu ya kufanya vitu kimiujiza au wazungu wanasema "SPIRITUAL POWERS". Kwahiyo basi nywele zinaumuhimu sana kwetu zaidi ya kutupatia muonekano mzuri.
Katika dunia hii, binadamu ndicho kiumbe pekee ambacho nywele zinakua "GROW" kichwani pale tu ukuaji unapoanza. Na iwapo nywele hizo zikiachwa bila kukatwa hukua kwa kiwango fulani kabla ya kuafikia kikomo. Urefu huo huo hutofautiana kulingana na mtu na mtu. Kwa mujibu wa utamaduni wa yoga"YOGIC TRADITION", Nywele ni zawadi "wonderful gift of the nature" ambayo husaidia kuongeza nguvu ya ndani ya mwili ambayo kila mtu anayo " kundalin energy"

 Picture
 
 Iwapo utaacha nywele zako zikuwe mpaka mwisho na kujiviringisha kwenye kichwa nguvu ya Uhai " Life force" itashuka toka kichwani kwako mpaka chini ya uti wako wa mgongo. Jinsi nguvu hizi zinavyoshuka chini ya uti wako wa mgongo ndivyo ambavyo uwezo wako wa kujibalance unavyozidi. Tuachane na mambo ya YOGA, na tujiulize je ni vipi na kwanini nywele zilianza kukatwa?

.

Ni lini na kwanini nywele zilianza kukatwa?

Picture
Historia inaonyesha kwamba miaka mingi sana iliyopita naongelea karne zilizopita, watu kutoka makabila na tamaduni mbalimbali walikua hawakati nywele. Nafikiri hili lipo wazi, angalia vizuri kwenye biblia na kuruhani au historian ya watakatifu na mitume na ma generous wa zamani na wasasa. Lakini watu hao wa zamani walikua wanakata nywele zao tu kwa lazima kama alama ya utumwa katika kipindi cha kukamatwa na utumwa wao. Hii ni kwa sababu kwa kipindi hicho wakamataji walielewa kwamba kulikua na aina fulani ya nguvu halisia ambayo ingepungua na kuzidhibitiwa iwapo nywele hizo zingekatwa .
 
Picture
Kwa mujibu wa historia ya watu wa China, mifupa ya sehemu ya mbele ya kichwa hupitisha mwanga kwenda kwenye glands za uti wa mgongo. Kupita huko kwa mwanga husaidia kuweka balance kati ya glandi za Thyroid na Pineal zilizopo kwenye uti wa mgongo. Hii husaidia ufanyaji mzuri wa kazi ya ubongo na ambayo mwisho wa siku husaidia katika kubalance homoni ya thyroxine na homoni za uzazi (sexual hormone). Kutokana na hilo China ilipotawaliwa na Mfalme Genghis Khan alikua akifahamu uwezo mkubwa wa akili ya watu wa China kutokana na nywele zao hivyo akawa anawalazimisha wanawake wote kukata mtindo wa nywele kama wa mdada hapo kushoto kwenye picha. Na ni mtindo ambao mpaka leo hii watu wanautumia bila kufaham origin yake.
.

Baada ya maka kupita ufahamu wa umuhimu wa nywele ulipotea. Ukataji wa nywele ukawa ni kitu maarufu sana, hali iliyosababisha kuvumbuliwa kwa mitindo mbalimbali ya nywele.
 
Sayansi inasemaje?
Picture
 
Nywele zinapokua kwenye kichwa na kufikia ukomo wake "maximum length" madini ya calcium, phosphorous na vitamin D hutengenezwa kwa wingi. Vitu hivi huingia kwenye mfumo wa mwili "Lymphatic fluid" na kwenye uti wa mgongo kupitia mirija iliyopo kwenye sehem ubongo. Kitendo hichi husababisha ukuaji mzuri kumbukumbu, nguvu ya mwili, stamina na utulivu.
 
Vilevile nywele hufanya kazi kama antenna ambayo husaidia kupitisha miale ya jua "sun energy" kwenda sehem ya mbele ya ubongo inayohusiana na kuona na kutafakari.

Iwapo umeamua kukata nywele zako, hautapoteza virutubisho peke yake bali utapoteza uwezo na nguvu zako, hivyo mwili wako utaanza kufanya kazi ya ziada ya kukuza upya nywele zako zilizopotea. Inaweza chukua miaka mitatu kutoka unapokata nywele zako mpaka zinapofikia ukomo wake.
Embu linganisha uwezo wako wa kutafakari na wa mke wako au girlfriend wako, mnalingana au kunakitu amekuzidi. Hakuna mchawi zaidi ya nywele zake ndefu asizozikata.

Nguvu ya nywele kwenye mwili

  • Nywele mbichi

Nywele zikiwa mbichi lazima zikaushwe ili kuepusha kuumwa na kichwa, vilevile unapoacha nywele zako mbichi husababisha kukatika katika. Uamuzi mzuri ni kukaa kwenye jua na kuacha nywele zako zikauke badala ya kukimbilia hair driers. Ukikaa kwenye jua nywele zitasaidia mwili wako kupata vitamin D.
Osha nywele zako mara unapopoteza mudi au ku-pata stress, hii itasaidia kutuliza stress na mood yako na kukurudisha katika ubora wako. Hii ndiyo maana huko India kuna utamaduni wa kuosha vichwa mara baada ya kutoka kwenye misiba. Umeipata hiyo?
  • Kuchana nywele kwa chanuo la mti/ mbao.

Picture
Miaka ya nyuma mama zetu na dada zetu au hata wazee wetu walikua wanachana nywele zao kwa kutumia chanuo la mti. Je, unafahamu njia hii ina umuhimu gani?
 
Ukichana nywele zako kwa chanuo la mti atleast mara mbili kwa siku inasaidia sana kuboresha mzunguko wa damu kichwani na kuisisimua. Ni option nzuri zaidi kutumia chanuo la mti badala ya kutumia chanuo la plastiki.
  Unapochana nywele zako kutokea mbele kwenda nyuma, nyuma kwenda mbele na kushoto kwenda kulia kwa mara kadhaa husaidia kupata msisimko na burudani. Kama ulikua umechoka hii ndiyo njia rahisi ya kuto uchovu.

Vilevile uchanaji huo wa nywele atleast mara mbili kwa siku huweza kuwasaidia wanawake kupata mzunguko mzuri wa hedhi, kuona vizuri na kuwa na mvuto na mchangavu wakati wote.  Kwahiyo kama wewe ni mwanamke achana na mambo ya mawigi na wivings.

Itaendelea...

Majambazi waua Askari...Wapora fedha Benki ya NMB

Tokeo la picha la ak 47
Watu kadhaa wanao daiwa kuwa ni majambazi jana  walivamia Benki ya NMB tawi la Mkuranga mkoani Pwani na kupora fedha kisha kumuua askari mmoja na kutokmea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafary Mohamed alithibitisha jana  jioni  kupata taarifa za tukio hilo.
 “Taarifa hizo nimezipata kuwa watu hao wanaodhaniwa majambazi wamevamia  Benki ya NMB, Mkuranga na kupora fedha ambazo kiasi chake bado hakijafahamika kisha kumuua askari mmoja aliyekuwa nje ya uzio wa eneo hilo la benki," alisema Jafary  .
Hata hivyo alisema askari aliyeuawa   hakuwa kazini ila walinzi wote wa benki wapo salama na silaha zao hazikuchukuliwa.
 
Mashine ya BVR Yaibiwa Jijini Mwanza, wawili watiwa mbaroni

Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana, waliiba mashine moja inayotumika kwa ajili ya kuandikishia vitambulisho katika daftari la kudumu la wapiga kura (BVR) katika kata ya Kayenze wilayani Magu mkoa wa Mwanza.
 
Akizungumza na mwandishi wetu, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, amesema mashine hiyo pamoja na nyingine 13, zilienda kuchajiwa katika nyumba ya kulala wageni ya BM Lodgei, lakini asubuhi zilipofuatwa haikuweza kupatikana.
 
Kamanda Mkumbo amesema baada ya kupata taarifa ya kuibiwa mashine hiyo, msako mkali ulifanyika ukiwamo wa kuwahoji wasimamizi wa mashine hizo.

Anasema baada ya kufanyika msako mkali kwa kuweka vizuizi sehemu mbalimbali, walifanikiwa kuikuta ikiwa imetelekezwa njiani ikiwa salama bila kuharibiwa, lakini hakuna mtu aliyeweza kukamatwa.
 
Hata hivyo, kamanda Mkumbo amesema polisi wamefanikiwa kuwashikilia watu wawili wa nyumba hiyo ya kulala wageni kwa mahojiano ili kufahamu mashine hiyo ilivyoweza kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
 
Aidha, ametoa wito kwa waandikishaji kuwa makini pale wanapohifadhi mashine hizo ili zisiweze kuharibiwa ama kuibiwa na watu wengine.
 
souce: mpekuzi blog
 
NYWELE NDEFU ZINAUMUHIMU GANI ?