Saturday, June 27, 2015

Tangazo la kuitwa kwenye usaili kwa wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2014

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014
ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Majina pia yapo kwenye tovuti ya TAMISEMI www.pmoralg.go.tz na Ofisi ya Kamanda wa Polisi
wa Mkoa/Wilaya iliyo karibu nawe ukatazame endapo jina lako ni miongoni mwa walioitwa
kwenye usaili.
Usaili utafanyika katika miji ya makao makuu ya mikoa Tanzania Bara Kwa tarehe
zilizooneshwa kwenye jedwali kwenye link hapo chini
Ni vema ukachungulia shule za katani kwako ili ukimwona mhusika apewe taarifa ili akashiriki.
Usaili utaanza 03.07.2015

No comments :

Post a Comment