Na. Emanuel
Utangulizi
Kahawa ni kinywaji kinachotumiwa na watu wengi duniani. Kwa mujibu wa jarida la Worldatlas takwimu za mwaka 2013 kati ya nchi kumi zenye matumizi makubwa ya kahawa, nchi inayoongoza zaidi kwa matumizi ya kahawa ni Finland ambayo ina wastani wa vikombe 2.64 vya kahawa vinavyonywewa kwa siku (kilo 9.6 kwa mwaka) kwa kila raia. Nchi zingine tano zinazoongoza kwa matumizi ya kahawa ni Norway namba 2 (Kilo 7.2 kwa mwaka)), Netherland namba 3 (Kilo 6.7 kwa mwaka), Slovenia 4 (kilo 6.1 kwa mwaka) , na Austria namba 5 (kilo 5.5 kwa mwaka) kwa kila raia.
Kuna mambo mengi huwa yanazungumzwa kuhusu kahawa. Mengine ni ya kweli na mengine si ya kweli. Leo hii nitaongelea vyote hivyo ili kuweka uwazi kuhusu kahawa.