Wednesday, July 22, 2015

TABOA NJIA PANDA

                                 
KITENDO cha serikali kupandisha kodi ya mabasi kutoka asilimia 10 hadi 25, kimezua sintofahamu kwa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) na hata kutishia kugoma. 
Wakizungumza leo jijini Dar es Salaam, katika mkutano mkuu wa mwaka wa TABOA, wajumbe wa chama hicho wamesema, wameshangazwa na hatua ya serikali kupandisha

AMISOM YAUKOMBOA MJI WA GEDO SOMALIA

Mji wa Baardheere ulioko eneo la Gedo nchini Somalia umekombolewa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika AMISOM, ikiwa ni mara ya kwanza kwa miaka saba.
Wapiganaji wa Al Shabaab wamekua wakiuthibiti mji huo tangu mwaka wa

ZIARA YA OBAMA: ANGA YA KENYA KUFUNGWA

                     
Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.


MACHALI AKABIDHIWA KADI YA ACT-MAENDELEO

                       Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto
Kasulu. Mbunge wa Kasulu Mjini ,Moses Machali amekihama rasmi chama hicho na kujiunga na ACT - Wazalendo huku akiwaeleza wananchi waliofika kumsikiliza katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kiganamo mjini hapa kuwa hatasita kuachana na chama chake kipya endapo kitaonekana kinatetea mafisadi na viongozi wanaokandamiza demokrasia.

Mbunge Wa Karatu kwa Tiketi ya CHADEMA Ajitoa Rasmi Katika Siasa

                   
Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji  Israel Natse, amejitoa rasmi katika siasa na kurudia kazi yake ya uchungaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini.


Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu ya kiganjani jana, alisema makubaliano

Wabunge Chadema waangukia katika kura za maoni

                          Wanachama wa Chadema wilaya ya Mbeya Vijijini
Dar/mikoani. Kura za maoni ndani ya Chadema zimeanza kuwa chungu kwa baadhi ya wabunge. Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akoonay na mwingine wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Kinondoni) jana waliangukia pua, huku mwenzao wa Karatu, Mchungaji Israel Natse akitangaza kuachana na ubunge na kurejea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

CHADEMA YAFANYA MAAMUZI

                         Mbunge wa Kahama, James Lembeli akizungumza na

Dar/Mikoani. Baada ya vuta vikuvute ya muda mrefu, hatimaye leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano maalumu utakaofanyika jijini Mwanza.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi na makao makuu zilisema kuwaa leo mgombea huyo atatangazwa mkoani hapa huku zikibainisha kuwa anayepewa nafasi kubwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.

MBUNGE AFARIKI

MBUNGE wa viti maalum ( CCM ), mkoa wa Dodoma Mariam Mfaki amefariki dunia leo katika hospitali kuu ya mkoa wa Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo hicho mjini hapa mtoto wa marehemu, Mohamed Mfaki amesema kuwa mama yake alilazwa juzi usiku hospitalini hapo akisumbuliwa na tatizo la kansa ya utumbo na mapafu.

PWANI: JESHI LA POLISI YANASA SILAHA ZA MOTO

                        Kamishna wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani, ACP Jafari Ibrahim akionesha silaha zilizokamatwa na jeshi hilo katika mapori ya mkoa huo
JESHI  la Polisi mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wasamaria wema, limefanikiwa kukamata silaha mbalimbali zinazotumika katika matukio ya kihalifu katika mapori ya mkoa huo.Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Jafari Ibrahim, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) amesema, 

CHADEMA: MATOKEO YA KURA KWA WALIOOMBA KUWANIA UBUNGE


MATOKEO YA KURA KWA WALIOOMBA KUWANIA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA NI HAYA YATUATAYO;