Sunday, June 28, 2015

UNAMFAHAMU KIUMBE MWENYE FURAHA KULIKO WOTE DUNIANI?

Kwa muhibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Programu za mazingira (United Nations Environment Programme -UNEP) kuna aina zipatazo million nane, laki saba za viumbe waliopo  Duniani. Kati yao wanyama wapo wa aina million 7.77, Mimea ipo ya aina 298,000, Fungus wapo wa aina 611,000 na Protozoa wapatao 36,400.

 
 
 
Kati ya viumbe wote hao kuna mnyama mdogo anayepatikana nchini Australia anayeitwa Quokka ameonekana kuwapiku wengine wote kwa kuchaguliwa kuwa ni mnyama mwenye furaha kuliko wote Duniani.
 
Mnyama huyu amekuwa akipendwa sana na watu mbalimbali hususani watalii katika upiga naye picha kutokana na uwezo mkubwa wa kuonyesha sura yenye furaha au tabasamu.
 
 
 
 
Quokka siyo mnyama mkali, nanirahisi sana kuanzisha naye urafiki. Kutokana na hili wanyama hawa wamepungua kwa kiasi kikubwa sana mara baada ya mbwa mwitu kuvamia misitu ya Australia.
Kwa sasa ni kati ya wanyama hadimu duniani na hatua mbalimbali zinachukuliwa ili kukinusuru kizazi chao.


 


 
 
 
 
 
 

 

 


Hii Hapa Taarifa Kamili ya ‘Magaidi’ Morogoro na Picha za Vitu Walivyokamatwa Navyo



Ripoti hii ni ya ITV June 27 2015 kutoka Morogoro inahusu watu watatu kufariki katika mapambano na Polisi, huku wawili kati yao wakihisiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Breaking News nyingine kuhusu tukio hilihili iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi inahusu watu sita kukamatwa na wengine 50 wanatafutwa, walikutwa wakiwa na sare za majeshi pamoja na silaha kama majambia kwenye msitu Mvomero.

Kwenye taarifa iliyofatia kutoka Mwananchi, imesema Mkulima Cassian Peter amefariki mchana wa June 27 2015 kwenye Hospitali ya Bwagala ambapo Polisi mmoja amelazwa na hii ni baada ya kujeruhiwa na hao watuhumiwa wa Ugaidi kabla hawajakamatwa

 Mtangazaji na Mwandishi wa habari wa Radio One Maulid Kambaya kwenye page yake ya Facebook alipost picha za walivyokamatwa navyo ‘Magaidi’ hawa


NCCR- Mageuzi Wasema Hawana Mpango wa Kujitoa UKAWA

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema hakitajitoa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na kuwapo kwa vikwazo vya ugawaji wa madaraka ndani ya umoja huo.

 Akizungumza katika kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho kilichoketi jana katika Hoteli ya Travertine jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, alisema lengo la umoja huo lilikuwa ni kuunganisha nguvu ili kuwa na sauti moja ya ushirikiano.

“Yapo maneno mengi yamesemwa na waandishi, wachochezi  wanasema NCCR inataka kuvunja Ukawa, tangu lini mama akakata mkono wa mtoto wake?
 
“Kama kuna wenye wazo la sisi kujitoa kwenye umoja huu ni vizuri watambue kuwa hatuna  mpango huo, na hili ni azimio lililotolewa na wajumbe wa Halmashauri Kuu. Pia itambulike kuwa chama hiki ni zao la Ukawa, hivyo si jambo rahisi kujitoa,” alisema Mbatia.

  Alisema Ukawa si sehemu ya kugawana madaraka na kudai kuwa umoja huo unaangalia zaidi masilahi ya wananchi.

Mbatia alisisitiza pamoja na uchochezi uliopo na changamoto ya ugawaji majimbo, wanaamini watavuka kwa kuwa lengo ni kusaidia wananchi na si vyama husika.

 Alisema umoja huo umejipanga vizuri, hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi  kwakuwa wana uwezo wa kutoa rais pamoja na viongozi wengine watakaounda Serikali.

Ajitosa  Sakata  la  Zanzibar

Aidha Mbatia alishagazwa na hatua ya Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuvunja Baraza la Wawakilishi juzi bila tukio hilo kuhudhuriwa na Makamu  wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad  baada ya wabunge na wawakilishi kumkatalia kuhudhuria.

 “Nimeshangaa sana rais wa Zanzibar anavunja Bunge yupo mwenyewe  bila Maalim Seif. Nini maana ya Serikali ya Umoja wa Kitafa?” alihoji Mbatia.
 
Alisema wanachama wa vyama vya CCM na CUF wanapaswa kutambua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni makubaliano  na mali ya Wazanzibari wote na si wanasiasa pekee.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa uandikishaji wa daftari la wapigakura unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kutumia mfumo wa kielektroniki (BVR), alisema hakuna dalili za daftari hilo kukamilika kwa wakati kutokana na kasi ndogo ya uandikishaji.

Alisema kutokana na hali hiyo, kuna viashiria vinavyoonyesha uchaguzi utakaofanyika Oktoba hautakuwa huru na wa haki.

“Uchaguzi hautakuwa huru na haki kwa sababu wameshindwa uandikishaji, kama leo wanasema kuna zaidi ya watu 5,000 wamejiandikisha mara mbili, wanamaanisha nini kwa wananchi?

“Tulishauri tangu mwaka jana kuhusu utaratibu wa uandikishaji na muda wa kuanza, lakini wenzetu wakawa wanabisha. Kwa hapa tulipofikia lolote likitokea  wa kulaumiwa ni Serikali ya CCM,” alisema Mbatia.

Alisema hadi sasa kuna baadhi ya mikoa ikiwamo Dar es Salaam na Pwani bado hawajaandikishwa. Pia NEC inapaswa kuwa na muda wa kuhakiki  majina ambako kutafanywa na wananchi.

Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya nne tangu ilipoingia madarakani mwaka 2005  imekuwa ikipoteza mvuto siku hadi siku kutokana na kutowajibika kwa ufasaha.
 
Alisema hadi sasa kuna mazingira ambayo mtu yeyote makini ni rahisi kuona jinsi Serikali ya CCM ilivyopoteza utashi, mvuto  na mwelekeo wa kuongoza Watanzania.

Mafuriko Ya Lowassa Yatua Jijini Dar......Kingunge Amwaga Wino Hadharani Kumdhamini, WanaCCM 212,150 Wajitokeza Kumdhamini

WAZIRI  Mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa amepata udhamini wa kishindo katika mkutano uliofanyika jana  katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni.
 
Lowassa alipata udhamini huo baada ya wanachama kujitokeza katika ofisi za Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni, Dar, ambapo alipata zaidi ya wadhamini  212,150 huku akisema Dar  imevunja  rekodi  ya mikoa yote ya Tanzania.
Akizungumza na maelfu ya wananchi waliofika katika mkutano huo Lowassa alisema kuwa amefurahishwa na watu waliojitokeza kumdhamini kwa kishindo kikubwa na hivyo hatavunjwa moyo  na maneno ya watu yanayovumishwa  kuwa anawapatia fedha ili wafike kwenye mkutano wake .
  Lowassa aliongeza kuwa anawaomba Watanzania wampe ridhaa ya kuwa rais wao kwani atahakikisha mianya yote ya rushwa na utendaji mbovu  wa kusuasua anausimamia kwa haki na weredi na ndani ya miezi sita tayari matokeo yatakuwa yameonekana.
  “Nawaombeni wananchi mnipeni ridhaa ya kuingia ikulu yaani nitahakikisha mianya yote ya rushwa na ufisadi nautokomeza, muyapuuze maneno na minong’ono ya watu kutaka kunichafua,” alisema.
 
Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisani fomu ya udhamini mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono mgombea huyo. 
 
Zoezi hili lilifanyika jana jioni ya Juni 27, 2015 kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni, Mkwajuni Jijini Dar ambapo Lowassa  alipata  jumla  ya  Wadhamni 212, 150 na kuifanya Dar es salaam kuwa Mkoa wa kwanza kuwa na idadi kubwa ya WanaCCM waliomdhamini

UTUMIAJI WA UNGA WA DONA ISIYOTENGENEZWA VIZURI NI HATARI KWA AFYA YAKO



Na Mtaalamu wa chakula

Utangulizi
Unga wa mahindi ni chanzo kikubwa cha virutubisho kwa watu wengi Barani Afrika. Virutubisho kama vile wanga, protini, madini na vitamin hupatikana kutoka kwenye mahindi au unga wake.
Unga wa dona ni unga unaopatikana kwa kusaga mahindi bila ya kukoboa. Siku za hivi karibuni kumekua na uhimizo mkubwa sana wa matumizi ya unga wa dona na kufanya watu wengi kuanza kupunguza taratibu matumizi ya unga sembe au uliokobolewa.

Faida za unga wa dona
Unga wa dona ulioandaliwa vizuri huwa una faida nyingi sana zaidi ya hata unga ambao umekobolewa. Faida hizo ni za kiuchumi au hata za kiafya. Faida ya kiuchumi ni kwamba Ukisaga mahindi au nafaka zingine bila ya kukoboa unapata unga mwingi kwa kila kilo utakayoisaga. Hii ni kwa sababu ukoboaji wa mahindi kunapoteza kiasi fulani cha unga. Faida zingine kiuchumi ni uandaaji kuwa rahisi zaidi katika ngazi ya familia. Kwa upande mwingine wa faida za kiafya za unga usiokobolewa kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta, protini, madini, vitamini, na nyuzinyuzi (fibre). Kwahiyo, unaimarisha zaidi lishe ya mlaji. Kama watu watajenga tabia ya kula mahindi ya kuchoma, kuchemsha au kupika kande pia wanapata faida kubwa ikiwemo kupata choo kikubwa mara kwa mara.

Udhibiti wa ubora katika hatua za utengenezaji wa unga wa dona
Dona yenye ubora na usalama inaweza kupatikana iwapo tu kunaudhibiti wa ubora katikatika mchakato wa utengenezaji. Udhibiti huo unatakia kuanzia mashambani, uvunaji, uhifadhi wa mahindi, hadi usagaji.

Nafaka zisipo vunwa, kukaushwa vizuri na kuhifadhiwa katika hali nzuri huweza kushambuliwa na wadudu waharibifu na vijidudu kama vile "fangasi" ambao mwisho wa siku huweza kusababisha nafaka au zao la nafaka kupungua ubora wake na kupata uambukizo wa "sumu kuvu" au kwa kitaalamu "aflatoxin". Aflatoxin huweza kuleta madhara makubwa kwenye miili ya binadamu kwa kusababisha cancer.

Vile vile iwapo udhibiti wa ubora hautazingatiwa katika hatua za uhifadhi hasa kwenye kuweka dawa za kuhifadhia mahindi "viatilifu" na usagaji wa mahindi. Kunauwezekano mkubwa sana kwa unga wa dona kubakiwa na kiwango kikubwa cha viatilifu au madawa ya kuhifadhia. Madawa hayo yanaweza kuwa ni sumu ambazo zinaweza zikamletea madhara makubwa mtumiaji wa unga huo. Kutokana na hilo basi ni muhimu nafaka zikahifadhiwa kwa mda unaofaa mara baada ya kuwekewa dawa kabla hazijafanyiwa mchakato mwingine wa kusagwa au kukobolewa.
Katika mashine za kusaga unga zilizopo kwenye maeneo yetu tunayoishi, suala la kuosha mahindi huwa halitiliwi maanani sana. Kutokana na ukweli kwamba mahindi mengi huwa yana kuwa na mabaki ya viatilifu suala la kuosha mahindi linatakiwa kuwa ni la lazima ili kuweza kuondoa au kupunguza kiwango cha madawa kilichopo kwenye mahindi.

Suala jingine la kujiuliza ni kwamba mara nyingi pumba za mahindi ndicho chakula kikubwa cha mifugo, lakini kiuhalisia sehemu ya nje ya nafaka/pumba za mahindi ndiyo sehemu ambayo huwa ina kiwango kikubwa zaidi cha dawa ili kuwazuia wadudu waharibifu. Kwahiyo mwisho wa siku sumu hizo huweza kuturudia kupitia mifugo.
Nini cha kufanya?
1. Ili kuweza kuepukana na madhara haya ya sumu za kuhifadhia nafaka na sumu kuvu ni budi kwa watanzania kurudisha utamaduni wetu wa zamani wa kujiandalia vitu vyetu wenyewe. Andaa mahindi yako mwenyewe kwa kuyaosha na kuyakausha vizuri kabla ya kusaga badala ya kwenda dukani na kununua. Dona ambayo hujui imeandaliwaje kabla ya kusagwa inaweza ikakuletea madhara makubwa zaidi ya faida ulizodhani ungezipata. Baada ya kusaga unga hakikisha unaukasha vizuri kabla ya kuhifadhi.

2. Kupunguza matumizi ya pumba kwa mifugo, na kuanza kuipa vyakula muhimu au mbadala kama vile nyasi badala ya kuilisha pumba, kwani pumba hizo huwa zina masalia makubwa ya viatilifu.
Hitimisho

Kutokana na uwezekano mkubwa wa kubakia mabaki ya madawa ya kuhifadhia mahindi yanayokuwemo kwenye unga wa dona ambayo haijatengenezwa vizuri, ni bora kuendelea kutumia unga wa sembe kuliko kuendelea kutumia dona ambayo hatujui imeandaliwaje. Unga wa sembe unaweza kuwa ni salama na ukatuletea faida zaidi kwani ukoboaji husaidia kuondoa gamba la nje la nafaka za mahindi hivyo kusaidia kupunguza kiwango cha mabaki ya sumu au madawa yaliyokuwa yamewekwa wakati wa kuhifadhi mahindi.