Utangulizi:
Siagi ya karanga ni uji/laini mzito uliotengenezwa
kutokana na karanga zilizokaangwa na kusagwa.
Siagi hii inaweza kuongezwa utamu na vitamini. Siagi ya karanga inatumika kwenye mkate,
kupikia na kuchanganya na vyakula mbalimbali.
Viambaupishi: Karanga, mafuta yasiyoganda, chumvi, sukari
‘stabilizer’ Lecithin
Vifaa: Mashine ya kusagia, sufuria, jiko la mkaa,
mwiko, mzani wa kupimia.
Hatua za uzalishaji:
1. Malighafi
Chagua karanga zilizokomaa,
kavu na zenye ukubwa unaofanana. Angalia zisiwe na ukungu kama vile “Aspergillus flavus”. Karanga ziwe na mafuta asilimia
2. Kusafisha
na kuchagua
Peta karanga kutoa uchafu na takataka zilizomo- toa karanga mbovu na zile zilizosinyaa au
kushambuliwa wadudu/ chembechembe
Kaanga kwa uanglifu kwenye joto la kutosha
ili karanga ziive
bila kuungua, ha tua hii inazipa karanga rangi ya kikahawia kidogo na kuleta harufu nzuri.
4. Toa ganda
Toa maganda kwenye karanga na kutoa zile zilizoungua
.
5. Saga
Saga
karanga mpaka kufikia ulaini unaotakiwa.
Chemsha siagi kufikia joto la 80o C – 90o C, changanya na mafuta sukari chumvi asilimia
na “stablizer” NB stablizer inawezkuongezwa
wakati wa kusaga karanga (wakati wa kurudia).
Kwenye chupa safi zilizochemshwa na kukaushwa. Ijazwe huku ikikorogwa ili kutoa hewa. Acha nafasi kidogo juu na funga kabisa hewa isipite. Unaweza ukaweka mafuta sehemu ya juu kwa kiasi kidogo ili kuzuia hewa isiingie kwenye siagi yako.
Imeandaliwa na Mtaalamu wetu wa Chakula.