Friday, June 26, 2015

SIASA ZINAVYOZIMALIZA PROFESSION ZA WATU

Na Mwandishi wetu:
Kusoma sana na kutoka kimaisha ni vitu ambavyo havina uhusiano kwa maisha ya sasa.. Hali hii inajidhihirisha katika maisha yetu ya sasa ambapo watu ambao hata hukutegemea pengine walifeli kabisa darasani lakini ndo hao wanaotufanyia fujo mitaani kwa fedha zao nyingi zisizo na kiwango


. Nikisema chafu simaanishi kwamba siyo halai au hazifai bali namanisha zinaweza kuwa zinafaa au hazifai, halali au siyo halali.

Nimefikia hatua ya kuandika habari hii kutokana na jinsi navyoona maisha yalivyobadilika. Maisha yamekua "opposite" na jinsi ilivyokua awali "Enzi za mwalimu" ambapo wasomi ndio walikua wanatesa. Sasa hivi fani au usomi siyo dili tena kwani kinachomata sasa hivi ni kile ulichonacho a.k.a mitonyo. Hata kama una PHD na masters zilizojaa Rambo watu hawatathamini hizo PHD iwapo hawatakuona unamafanikio yanayoonekana, namanisha assets kama vile nyumba, magari, n.k.

Nimekaa sana na kujiuliza ni kwanini wasomi wengi sasa hivi wanakimbilia kwenye siasa? je ni kweli wanataka kutukomboa kwenye shida zetu sisi walala hoi tuliokata tama au wanataka kujiondolea stress zao za profession zao zisizowalipa?Nafikiri msomaji wangu jibu unalo.

Kwa karne hii hakuna kazi inayolipa kama siasa. naandika hili nikiwa na "confidence" ya kutosha. Embu fikiria mbuge leo hii anakaa mjengoni kwenye full kiyoyozi na sofa seti kwa miaka mitano anavuta milioni 238 wakati professional mwenzangu mwalimu anakaa kazini miaka 30-40 kwenye kiti cha mbao na mazingira magumu maisha yake yote anapokea kiinua mgongo kisichozidi mil 20. Na hali hii haitokei kwa walimu tu, bali ni kwa profession wengi kama vile mahakimu, madaktari, polisi n.k Je hii ni haki? au wote tukimbilie kwenye siasa.

Leo hii tunaona utitiri wa"BONGO MUVI" wakitangaza nia ya kugombea ubunge. Nafikiri ni baada ya kuona mafanikio ya wenzao waliojaribu kama wakina Mh. SUGU. Sioni kwamba ni jambo baya, najua hilo linatokana na kusoma alama za nyakati.
Tukiangalia vizuri historia za Bongo muvi wengi za darasani utakuta baadhi yao ni wale waliokuwa "Back Benchers" ambao mwisho wa siku hawakuweza kuruka tuta la form4 au hata darasa la saba. Lakini kwa kipindi hichi wanajaribu kutumia "Popularity zao na Influence zao kuingia mjengoni". Mwisho wa siku akiingia mjengoni usishangae akakupiku wewe na professiona yako na vyeti vilivyojaa rambo.

Kwa jinsi hali inavyoendelea ni budi kwa serikali na wadau wengine kutafuta mbinu mbadala ya kuokoa profession za watu kwa kuboresha masilahi yao na kuhakikisha kwamba mzani hauegemei upande mmoja kwani mwisho wa siku hatuta weza kutofautisha kati ya siasa na biashara haramu, kwani watu watatumia mbinu chafu zitakazowaweka madarakani ili mwisho wa siku waweze kuneemeka na kuwaacha wananchi wanaangamia.

 

No comments :

Post a Comment