Juice nikinywaji kinachotokana na matunda yaliyokamuliwa. Kinywaji hichi hunywewa kwa ajili ya kuburudisha na kuipa miili afya. Ili kinywaji hiki kiwe na ubora na usalama ni lazima kichemshwe kwa kuzingatia joto na muda ili kuua vimelea kama vile bakteria na vimeng'enyo vilivyopo kwenye matunda. Kitendo hichi cha kitaalamu kinaitwa "PASTEURIZATION".
Katika grocery nyingi hapa Tanzania juisi nyingi huuzwa zikiwa hazijafanyiwa mchakato huu wa kuchemsha. Kinga yamiili huweza kudhibiti kiasi kidogo cha vimelea viletavyo madhara. Ingawa hii siyo ya kutegemea sana kwani wakati mwingine vimelea hivi huzidi uwezo wa miili kuvidhibiti hivyo kuleta magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa ya matumbo, kuharisha na kutapika. Mamlaka zinazohusiana na Vyakula na Madawa zinashauri juice zinazotengenezwa kwa ajili ya kutumiwa na makundi maalumu kama vile watoto wachanga, watoto wadogo, wamama wajawazito na wazee ambao kinga zao za miili zipo chini kutumia juisi ambazo zimechmeshwa ili kuepuka kupata madhara au magonjwa.
VIMELEA VINAWEZAJE KUINGIA KWENYE JUISI?
Kihalisia sehemu ya ndani ya tunda haina vimelea vya magonjwa. Vimelea vinavyochafua juisi hutokea kwenye mazingira ya nje kama vile hewa, mikono ya mtengenezaji, sehemu ya nje ya tunda n.k.
Watu wengi huzani kwamba kunywa jusi ambayo haijachemshwa "Natural" ni bora zaidi, lakini hii siyo kweli. Juisi ya aina hii inaweza ikakuletea madhara makubwa zaidi na kukufanya usipate faida ambazo ulizani ungevipata.
.
JE, INAWEZEANA KUTENGENEZA JUISI SALAMA KATIKA MAZINGIRA YA NYUMBANI?
Ndiyo! Unaweza kutengeneza juisi bora na salama nyumbani kwako kwa kuzingatia usafi wa kila kitu kama vile matunda, sehem ya kuandalia matunda, vifaa vya kutengenezea juisi kama vile visu, blender n.k.
Ndiyo! Unaweza kutengeneza juisi bora na salama nyumbani kwako kwa kuzingatia usafi wa kila kitu kama vile matunda, sehem ya kuandalia matunda, vifaa vya kutengenezea juisi kama vile visu, blender n.k.
Matunda yanatakiwa kusafishwa kabla hayajamenywa ata kama maganda hayo hautayatumia kwenye kuzalisha juisi yako. Sehemu ya nje ya matunda huweza kubeba bakteria ambao wanaweza kuingia kwenye juisi wakati wa kuandaa jusi yako hasa wakati wa kukatakata au kumenya.
Baada ya kutengeneza, juisi inatakiwa kuchemshwa kwa nyuzi joto 80-100 kwa muda usiozidi dakika 20. Joto hili na muda huo unafaa kwa ajili ya kuua vimelea. Iwapo Joto a muda utazidi juisi hiyo inaweza kupoteza virutubisho muhimu.
Video iliyopo hapo chini inatoa muongozo wa njia bora ya kuchemsha juisi .
No comments :
Post a Comment