Mabenki Nchini Ugiriki yanafunguliwa leo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha majuma matatu.
Kuna milolongo mirefu kwa sasa nje ya mabenki hayo, pale bunge la taifa hilo lilipopitishia masharti magumu juma lililopita kama sehemu ya kutatua matatizo yake ya kifedha.
Baadhi ya masharti yangali pale pale, ikiwemo viwango vya fedha ya mtaji kutoka mataifa ya ulaya.