Monday, July 20, 2015

JESHI LA POLISI LAFANIKIWA KUWAUWA MAJAMBAZI WATATU WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI CHA SITAKI SHARI NA KUWATIA WENGINE WAWILI MBARONI


MAJAMBAZI waliovamia Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la kukamatwa na
kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao  inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
 
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.
 
Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala,Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo ,Mkuranga.
 
Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15),Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.
 
Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki  15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi na kuweka kinyesi juu.
 
Amesema katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina ya  Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.
 
Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kwa kuwa halipi.
 
Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiklia na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nao.
 
“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari” amesema Kamishina Kova.
 
Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea  julai 12 majira ya saa nne.

Naibu wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari ,Tazara,jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
      
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.
  
 Fedha za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.

 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za majambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam 

Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo jijini Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment