Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amewataka wageni wasiokuwa na shughuli muhimu ya kufanya mkoani hapa kutokuja katika kipindi cha juma hili ili kuepusha usumbufu utakaojitokeza.
Misime alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu wiki hii ambayo inatarajiwa kuwa na ugeni mkubwa wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao