DODOMA: Kikao cha HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) kimekamilika na kufanikiwa kuwateua wagombea wake 3 ambao ni… 1) John Magufuli 2) Asharose Migoro 3) Amina Salum Ali
Kazi ya upigaji kura inaendelea hivi sasa katika mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC), ambapo majina matatu yatapatikana na kupelekwa katika mkutano mkuu utakaoanza majira ya saa 3:00 usiku.
Kuna habari zimeenea mitandaoni kwamba kuna mtu ambae amekamatwa na mabilioni ya pesa Dodoma, kingine ni kwamba amekamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.
Wapambe wa Mbunge wa Monduli Edward Lowassa hivisasa wanafanya maandamano makubwa nje ya ofisi za CCM hapa makao makuu ya CCM wakipinga Mbunge huyo kuchujwa katika tano bora.
Wapambe hao wanaimba nyimbo mbalimbali za kukiponda chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa chama hicho sio cha
Dar es Salaam. Kama alivyowashangaza wengi pale alipojitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais Mei 29 mwaka huu, ndivyo Dk John Magufuli alivyowashangaza tena jana kufikia hatua hii ya tano bora.
Bila makeke, majivuno wala majigambo, Magufuli ambaye ni
Habari za Hivi punde kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma ni kwamba wajumbe wa kamati kuu watatu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.
Akizungumza usiku huu majira ya saa saba za usiku Dkt. Nchimbi amesema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huu chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.
“Katika kikao cha leo kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha leo kimeonyesha kuminya wanaokubalika kwa manufaa ya wachache wasiokubalika” Amesema Dkt. Nchimbi.
Hivyo basi kwa sababu hiyo wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kuto kuyaunga mkono.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania zinaonesha kuwa mgombea anayekubalisa sana CCM ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe.
Dodoma. “Anakatwa, hakatwi” ndilo swali lililokuwa linaulizwa nchi nzima jana, lakini hatimaye Kamati Kuu ya CCM iliyokutana hadi usiku wa manane iliibuka na jibu kwamba Edward Lowassa amekatwa, huku kukiwa na wingu zito baada ya wajumbe watatu kupingana na uamuzi huo.