Friday, June 26, 2015

JINSI YA KUTENGENEZA SIAGI YA KARANGA-PEANUT BUTTER


 
 

   Utangulizi:
Siagi ya karanga ni uji/laini mzito uliotengenezwa kutokana na karanga zilizokaangwa na kusagwa.  Siagi hii inaweza kuongezwa utamu na vitamini.  Siagi ya karanga inatumika kwenye mkate, kupikia na kuchanganya na vyakula mbalimbali.
Viambaupishi: Karanga, mafuta yasiyoganda, chumvi, sukari ‘stabilizer’ Lecithin
 
Vifaa: Mashine ya kusagia, sufuria, jiko la mkaa, mwiko, mzani wa kupimia.
Hatua za uzalishaji:
1.   Malighafi             
 Chagua karanga zilizokomaa, kavu na zenye ukubwa unaofanana.  Angalia zisiwe na ukungu kama vile “Aspergillus flavus”.  Karanga ziwe na mafuta asilimia
2.   Kusafisha na kuchagua  
Peta karanga kutoa uchafu na takataka zilizomo- toa karanga mbovu na   zile zilizosinyaa au kushambuliwa wadudu/ chembechembe
 
 3.    Kaanga.        
 Kaanga kwa uanglifu kwenye joto la kutosha ili  karanga ziive bila kuungua, ha tua hii inazipa karanga rangi ya kikahawia kidogo na kuleta harufu nzuri.
4.     Toa ganda
   Toa maganda kwenye karanga na kutoa zile zilizoungua
                                    .
5.     Saga                  
 Saga karanga mpaka kufikia ulaini unaotakiwa.
 6.     Changanya        
Chemsha siagi kufikia joto la 80o C – 90o C, changanya na mafuta sukari chumvi asilimia na “stablizer”  NB stablizer inawezkuongezwa wakati wa kusaga karanga (wakati wa kurudia).
 7.      Jaza   
 
Kwenye chupa safi zilizochemshwa na kukaushwa.  Ijazwe huku ikikorogwa ili kutoa hewa.  Acha nafasi kidogo juu  na funga kabisa hewa isipite. Unaweza ukaweka mafuta sehemu ya juu kwa kiasi kidogo ili kuzuia hewa isiingie kwenye siagi yako.
 
Imeandaliwa na Mtaalamu wetu wa Chakula.

   
 
 
 
 

6 comments :

  1. Ni aina zipi za karanga ndio nzuri kwa ajili ya kutengenezea peanut butter?

    ReplyDelete
  2. UMEEKA KATIKA VIFAA VYA KUTUMIA KATIKA UPISHI WA SIAGI YA KARAMGA IKIWEMO MZANI. ILA HUKUSEMA MATUMIZI YAKE NIKIMAANISHA HIVYO VIFAA TUTAPIMAJE ILI KUPATA UWIANO MZURI KATIKA MAPISHI YETU.PIA NINAOMBA UNIFAHAMISHE HIYO LECITHIN INAPATIKANA WAPI NA NI LAZIMA KUITUMIA KATIKA UPISHI WETU?

    ReplyDelete
  3. Sijakuelewa hapo kuchemsha siagi unachmsha hyo peanut au Na kama hauna hyo stabilizer kwn ni lazima

    ReplyDelete
  4. Kama Sina mashine ya kusagia karanga naweza nikatumia Brenda?

    ReplyDelete
  5. Naomba kujua aina ya mafuta unayoweza kutumia kuchanganyia na Kama no siagi basi ni siagi gani

    ReplyDelete