Monday, June 29, 2015

Watangaza nia ya Uraisi CCM wafika 42

Tokeo la picha la WATANGAZA NIA CCMMWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Banda Sonoko, jana amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho ili kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao akiwa ni mgombea wa 42.
Baada ya kuchukua fomu hiyo jana, Sonoko alisema kama chama hicho kitampitisha kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao na kushinda, moja ya vipaumbele vyake ni pamoja na kuzingatia misingi imara ya ilani ya 2005 pamoja na kuondoa umaskini kwa Watanzania.

Sonoko amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Temeke ambapo katika kampeni zake za kusaka urais atatumia kauli mbiu inayosema "Kutokomeza Umaskini".

Alisema akiingia Ikulu, atawatimizia Watanzania mahitaji mbalimbali ambayo wameyakosa muda mrefu ambapo yeye ana sifa zote za kuwa rais ndio maana ameamua kuchukua fomu.

Aliongeza kuwa atahakikisha nchi inaendeshwa kwa kodi za wananchi si misaada kutoka nchi wahisani ambapo wanawake watawezeshwa katika mambo mbalimbali na kupewa nyadhifa kwenye vyombo vya maamuzi pamoja na vijana.

Sonoko alisema Serikali ambayo ataiongoza itasimamia haki, kupinga vitendo vya utoaji na upokeaji rushwa hasa Mahakamani ambapo kesi zitakuwa zikiendeshwa kwa muda maalumu, kurudisha viwanda, kuinua kilimo na kuboresha miundombinu.

"Nitahakikisha kila Wilaya inakuwa na sehemu yake ya kuegesha magari, kuongeza ajira na kuwasaidia vijana," alisema na kuongeza kuwa, hadi Julai mosi, mwaka huu, atakuwa amekamilisha taratibu za kupata wadhamini 450 katika mikoa 15.

NAFASI YA KAZI: Special Needs Teacher : Haven of Peace Academy (HOPAC)


The mission of Haven of Peace Academy (HOPAC) is to provide an excellent, Christ-centred, international education that meets western academic standards and equips students to live out a biblical worldview in all areas of life to the glory of God.
Haven of Peace Academy is seeking a Special Needs Teacher for the 2015/2016 school year. School year: August – June with classes Monday to Friday. HOPAC follows the Cambridge curriculum.
HOPAC, founded in 1994, is an international Christian K-12 school with over 300 students from 33 different countries and a variety of religious backgrounds including Christian, Muslim and Hindu. While the majority of students come from families of missionaries and the non-profit and international business community, one third are Tanzanian.
HOPAC teachers must be committed Christian, 55 years of age or younger with Bachelor degree, at least 3 years of teaching experience and fluency in English. HOPAC expects teaching staff to be supported spiritually and financially through a mission organization or home church. The school provides volunteer staff assistance in the form of a monthly living allowance that covers a significant portion of monthly in-country expenses.
Qualifications:
- Bachelors Degree
- Evangelical Christian
- 3+ years experience

How to apply

Please email Cover Letter and CV to personnel@hopac.net
Kindly state the job posting in the email subject line

Lipumba asema CCM hakiwezi kutoa rais mwadilifu

Mara. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema CCM hakina kiongozi mwadilifu atakayeweza kupeperusha bendera ya nchi, kutokana na viongozi wake kugubikwa na ufisadi.
Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo jana kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo mjini Musoma alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
Alisema lengo la mkutano huo ni kuwaelimisha wananchi kuchagua viongozi wenye uadilifu na wanaojali rasilimali za nchi na watu wake badala ya kuchagua viongozi ambao ni mafisadi na wasio na uchungu wa kuinua pato la Tanzania.
Alisema anaunga mkono kauli ya mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Makongoro kuwa CCM kimekamatwa na kimekumbatiwa na vibaka ambao hawataki kuondoka ndani ya chama kwani wamekwishaweka mizizi.
“Nyerere atambue kuwa vibaka wakishang’ang’ania hawatoki na hata hayati Baba wa Taifa angekuwa hai angekuwa upinzani, hakika nawaeleza,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema anawashangaa viongozi wa CCM ambao wanataka kuongoza nchi wakati walishindwa kuwatetea Watanzania katika Bunge la Katiba ili ipatikane Katiba bora.
“Hawa waliweka masilahi mbele na kulinda nafasi na madaraka ya viongozi, kumbe lengo lao ni kuendelea kuwanyonya wananchi,” alisema.
“Katiba ile ilikuwa inampunguzia madaraka rais na pia ilikuwa inawapa wabunge nguvu ya kuihoji Serikali, ilipinga waziri kuwa wabunge ili Bunge liwe huru kujadili Serikali,” alisema.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kujiandikisha kwa wingi na kuhakikisha kipindi cha kupiga kura kitakapofika, wachague wagombea wa Ukawa ili wanaodai kuwa haipo wapate kuijua.
Alisema kama isingekuwa sheria, vyama vyote vya upinzani vingekuwa chama kimoja na kupeperusha bendera ya Ukawa katika kuchagua viongozi kuanzia ngazi za udiwani, ubunge na urais.
“Nimetangaza nia nitagombea urais, lakini nasubiri kwanza Ukawa iamue ni nani anayefaa kugombea kupitia umoja huu, hata kama si mimi, nitahakikisha atakayepitishwa nitampigia kampeni ili nchi isiende kwa mafisadi,” alisema.


Zitto awatolea uvivu wanaomwita kibaraka wa CCM

Tanga. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kama angekuwa ni msaliti na kibaraka wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asingeweza kuongoza mapambano ya kuwang’oa mawaziri 13 kwa miaka mitatu katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mabawa uliolenga kukitangaza rasmi chama chake kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake.
Zitto alisema mwaka 2012 aliongoza mapambano ya kuwang’oa mawaziri wanane wakati mwaka 2013 walijiuzulu mawaziri wanne kwa kashfa ya Oparesheni Tokomeza, wakati mwaka jana, mawaziri watatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walilazimika kuachia ngazi kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta escrow.
“Wananchi wa Tanga jiulizeni, hivi msaliti anawezaje kuwang’oa mawaziri wote hao ndani ya kipindi cha miaka mitatu?” alihoji Zitto na kusisitiza kuwa kuna watu wamelenga kutumia hoja hiyo kwa lengo la kumchafua.
Akizungumzia lengo la kuanzisha chama cha ACT - Wazlendo, Zitto alisema ni kutokana na kunyanyaswa na kuonewa na viongozi wa ngazi ya juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hivyo aliona njia mbadala ni kutafuta jukwaa lingine la siasa ili aweze kuwatumikia Watanzania. “Kuanzisha chama kipya siyo kazi nyepesi, lakini kwa sababu tulikuwa na dhamira ya dhati tumeweza kufyeka mapori na sasa tumefanikiwa na leo hii tunakileta kwenu ili mkipokee kwa sababu ACT ni yenu,” alisema Zitto.
Alisema chama hicho kina mpango wa kuhamasisha ufufuaji wa zao la mkonge mkoani hapa ili lilimwe na wakulima wadogo badala ya wakubwa kwa sababu katika nchi zilizofanikiwa kuleta mapinduzi ya mkonge zimesaidiwa na wakulima wadogo.
Alisema kupitia ACT atahakikisha hoja yake aliyoiwasilisha bungeni na kupingwa na wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Tanga ya kulifufua zao la mkonge inatekelezwa.
Mjumbe wa ACT, Seleman Msindi maarufu ‘Afande Sele’ alisema hajajiunga na ACT - Wazalendo kwa sababu ya urafiki wake na Zitto, bali amebaini kuwa ndiyo chama chenye mlengo makini wa kuipeleka nchi kunakostahili mara kitakapofanikiwa kushika dola
Source: Mwananchi