Tuesday, July 21, 2015

Burundi:Uchaguzi wa urais umeanza


                           
Baada ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye raia nchini Burundi sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao. Watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura.
Mwaandishi wa BBC aliyeko nchini humo anasema kuwa, milio ya risasi na gruneti imesikika usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura.
Foleni katika kituo cha kupigia kura                  
Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.


Raia wameanza kupiga kura Burundi                        
Viongozi wanne wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.
Rais Pierre Nkurunziza, akiwaamevalia jezi ya michezo alipiga foleni katika kituo kilichokaribu na mji wa Ngozi alikozaliwa na kupiga kura.
Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi huu baada ya serikali ya Burundi kuwanyima vibali waangalizi wa Umoja wa Afrika katika muda wa lala salama.
Waangalizi wachache wameshiriki katika uchaguzi huo                           
Hata hivyo, waangalizi kutoka umoja wa Afrika Mashariki wapo huko kwa mwaliko wa rais Nkurunziza.
Karatasi za kura zinaonesha kuwa kulikuwa na wagombea nane wa kiti cha urais lakini wanne kati yao wameshathibitisha kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wakipinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Uchaguzi huu unafanyika licha ya taaruki kuhusiana na mgogoro wa kisiasa                      
Wagombea hao ni Agathon Rwasa, Jean Minani, Domitien Ndayizeye na Sylvestre Ntibantunganya.
Wapiga kura wanamchagua rahisi                            
Jina la rais Nkurunziza na ishara ya chama chake imechapishwa miongoni mwa wagombea wa urais.
Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi.
Mkuruzinza ameonekana akipiga kura mki wa Ngozi                               
Katika maeneo mengine risasi zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo.
Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo. Viongozi wa upinzani wamesusia kushiriki uchaguzi huo kwa dai rais anakuka sheria kwa kuwania muhula wa tatu
Kwa mujibu wa mshauri wa kisaisa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na 'magaidi' wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.
Viongozi wanne wa upinzani walisusia uchaguzi huo                           
Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Takribani watu 70 waliuawa wakati wa vurugu za kupinga uchaguzi huo                    
 Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.
Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu huku wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.

Source: BBC Swahili

No comments :

Post a Comment