Wednesday, June 24, 2015

TOMATO SAUCE


Utangulizi
Sosi ya nyanya ni kiungo kinachotumika ili kukoleza chakula wakati wa mlo. Sosi ya nyanya hutengenezwa kutokana na nyanya zilizoiva na ni viungo.
Jinsi ya kutengeneza:
Vifaa vinavyohitajika:
 Mashine ya kusagia
 Sufuria ya kuchemshia
 Mzani
 Vifungashio:- Chupa za sosi zenye mifuniko
- Lebo na ‘seal’
Mahitaji:
1. Nyanya zilizoiva gramu 900
2. Siki (vinegar) mls 50
3. Sodiumu Benzoate 750 ppm (750 mg/ kg)
4. Maji salama
5. Vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho ya unga, haradani (mustard n.k)
6. Chumvi
7. Sukari
8. Unga wa muhogo
 Hatua za Utengenezaji:
 Chagua nyanya zilizoiva vizuri zenye umbo la yai- nyanya za Tengeru ni nzuri zaidi.
 Osha kwa maji safi
 Menya na kuondoa mbegu (waweza pia pika na mbegu ingawa kuna wengine huwa hawapendi ladha na muonekano wa mbegu kwenye sosi)
 Katakata vipande vidogo na weka kwenye chombo cha kusagia.
 Saga vizuri kupata rojo
 Visage viungo( vitunguu, hoho, pilipili manga, vitunguu swaumu, binzari n.k kulingana na matakwa) na vifunge kwenye kitambaa safi.
 Kitumbukize kwenye maji kiasi na chemsha na kamua kitambaa ili kupata supu
 Changanya supu ya viungo, chumvi, sukari na mchanganyiko wa nyanya Chemsha mpaka upate uji mzito. Mara nyingi sosi inakua tayari iwapo uzito umebaki nusu ya uzito wa mchanganyiko wa awali au 26-28 digrii (26-280 brix)
 Ongeza kamikali (Sodium Benzoate, Vinegar) kisha chemsha kwa dk 5
 Paki kwenye vifungashio safi ikiwa bado ina joto nyuzijoto 80-90.

No comments :

Post a Comment