Tuesday, July 7, 2015

JINSI YA KUTENGENEZA ACHALI YA EMBE (MANGO PICKLE)

http://emanuelcosmas.blogspot.com/

1. Utangulizi:

Achaliya embe ni bidhaa inayotokana na usindikaji wa zao moja kwa kutumia chumvi.  Bidhaa hii ikisha sindikwa hifadhi yake inatokana na tindikali aina ya asetiki . Mazao mengine yanayoweza kutengenezwa achal ni kama Embe, ndimu, kabegi (kimchi), matango, shelisheli, uyoga n.k
 
 

2. Kanuni za usindikaji
Katika uzalishaji wa achali, chumvi inayotumika wakati wa kuchachua inafanya kazi ya kuhifadhi ikisaidiana na kuwepo kwa tindikali na sukari, mchanganyiko huu huzuia kukua kwa chembechembe waharibifu. Katika hali hii ya kuwepo kwa tindikali nyingi , kuchemsha bidhaa sio lazima.

3. Mahitaji

Sukari

Pilipili nyekundu

Haradali-mustard

Mafuta ya kupikia

Siki

Uwatu -fenugreek

Binzari kutegemea na matakwa.
 
4. Vifaa:
·         Ndoo ya plastic
·         Sufuria kubwa
·         Sufuria ndogo
·         Mwiko
·         Brashi
·         Visu-‘stainless steel’
·         Jiko
·         Meza ya stainless steel au alluminiamu
·         Mizani
·         Kinu, chekeche au grinder
·         Kibao

5. Vifungashio:

·         Chupa za kioo
·         Vizibo, vifuniko
·         Lebo
·         ‘Seal’
 
6. Hatua za Utengenezaji

Hatua:

Maelezo:
 
 
Vuna:
-          Maembe ambayo hazijaanza kuiva
 
 
Chagua:
-        Chagua maembe ambayo yana rangi ya kijani iliyokolea, maembe mabovu na yaliyoivaa   yasitumike
 
 
Osha:
-        Osha kutumia maji safi yaliyochemshwa na kupozwa kisha uache maji yachuruzike.
Katakata:
-        Kwa kutumia kisu cha ‘stainless steel’, kata ncha zote mbili za embe kisha katakata mara mbili au nne hadi tano kulingana na mahitaji.  Tumia vifaa visivyopata kutu (stainless steel, aluminium), visu na meza za kutayarishia.
 
 
Changanya:
-        Weka chumvi ,  koroga pamoja na maembe yaliyokatakatwa   kwenye ndoo.
 
 
Chachua:
-        Jaza kwenye ndoo ya plastic ukishindilia ili kuhakikisha kuwa hewa haibaki ndani. Maembe yaliyochachuka pamoja na chumvi huweza kukaa wiki 3-4 kabla ya kumalizia usindikaji. Baada ya kila wiki angalia kama chumvi bado ipo ya kutosha, ongeza asilimia 10% ya chumvi endapo imepungua.
 
 
Osha:
-                Osha maembe yaliyochachuka pamoja na chumvi kutumia maji safi.
-                Osha mara tatu hadi nne kuhakikisha kuwa chumvi imepungua.
 
 
Changanya:
   -Ongeza uwatu ‘fenugreek powder’:
-        Sukari
-        Haradali-‘mustard’
-        Pilipili nyekundu
-        Koroga ili kupata mchanganyiko unaofaa.
 
 
Tuliza:
-        Acha mchanganyiko huo kwa muda ili kuruhusu kukomaa kama dakika 15-30.
-        Hakikisha umefunika mchanganyiko wako
 
 
Ongeza:
-        Mafuta ya maji yasiyoganda (kama alizeti, pamba, karanga n.k. Mafuta yaliyochemswa na kupoa).
-        Ongeza siki
 

-   Binzari nyekundu kiasi kutengeneza rangi unayoitaka
           -Fungasha kwenye chupa safi kavu.
 

1 comment :

  1. maembe na chumvi ikae kwa muda gani ndio iwe tayari?

    ReplyDelete