Thursday, July 2, 2015

NJIA ZA HARAKA KUGUNDUA ASALI ILIYOCHAKACHULIWA

Na. Emanuel

Utangulizi

Asali ni zao au bidhaa linalotokana na nyuki. Ili nyuki waweze kuzalisha asali wanahitaji malighafi kama vile 'nectar" inayotokana na maua pamoja na maji. Wakati mwingine nyuki hutumia viambata vinavyotokana na majimaji miti " plant secretions". Nyuki anaweza kutembea hadi kilometa tano kutafuta maji na nekta kwa ajili ya kutengenezea asali.

Je, Unafahamu kwanini nyuki huzalisha asali?

Nyuki huzalisha asali  kwa lengo la kuweka akiba yake ya chakula kwa ajili ya matumizi ya baadae, hasa wakati wa uhaba wa chakula kama vile msimu ambao hauna maua ya kutosha ama kiangazi.

Faida za asali

Asali inafaida mbalimbali za kiuchumi na kiafya. Asali inakiwango kikubwa cha sukari "Carbohydrate' ambayo husaidia kuipa miili nguvu. Vilevile asali ina kiwango kikubwa cha madini, protini, vitamin n.k.
Katika sehemu nyingi duniani asali hutumika zaidi katika matibabu zaidi ata ya matumizi y chakula.
Asali vilevile hutumika kama chanzo cha sukari katika bidhaa mbalimbali kama vile wine na bia. Wakati mwingine asali hutumika kama malighafi katika kutengeneza bidhaa zingine kama vile vifungua kinywa, mikate n.k
  •   Aina za asali

 Kuna aina nyingi sana za asali. Aina hizo zinatokana na sababu mbali mbali kama vile;
1. Aina kutokana na chanzo cha asali
mfano:
> Asali inayotokana na nekta za maua (Blossom Honey)
>Asali zinazotokana na aina moja ya maua (Mono-floral Honey) mfano asali zinazotokana na maua ya alizeti na
 >Asali zinazotokana na mchanganyiko wa maua (Multi-floral Honey). Asali zinazotokana na maua ya aina moja huuzwa kwa bei ghali zaidi ya asali zinazotokana na maua ya aina nyingi-polyfloral.
2. Aina kutokana na matumizi ya asali- mfano: Asali ya mezani na asali za viwandani n.k
  • Njia za kujua asali iliyochakachuliwa 

"Nafahamu wewe ni mnunuaji mzuri sana wa asali. Umeshawahi kujiuliza asali unayonunua ni asali kweli 100% au kuna wajanja wamefanya mambo yao wanayoyafahamu?"

 Uchakachuaji wa asali hufanyika kwa lengo la kufanya udanganyifu kwa mnunuzi na kumuongezea faida muuzaji. Iwapo uchakachuaji utafanyika vizuri bila mnunuaji kutambua, muuzaji anaweza akapata faida zaidi ya mara mbili. 

Uchakachuaji unafanyikaje?

 Uchakachaji huweza kufanyika katika hatua mbalimbali kwenye mashamba au kwa wauzaji (Vendors).
"Najua wewe ni mnunuaji mzuri sana wa asali pale stendi ya singida, Dodoma n.k. "  
Mara nyingi uchakachuaji hufanyika kwa njia kuu tatu;
    1. Kuongeza sukari guru
    2. Kuongeza sukari iliyounguzwa/ Caramel"
    3. Kuongeza maji
     

Utajuaje kwamba asali imechakachuliwa?

Iwapo uchakachuaji wa aina hii utafanyikan utafanyika zipo njia tano rahisi za  kugundua udanganyifu huu. Njia hizo ni hizi zifuatazo;
 1. Mimina asali kidogo katika chupa ya maji safi.
 Iwapo maji yatachafuka (kuchukua rangi ya brown au rangi ya asali) ujue asali hiyo inakitu kingine imefanyiwa mambo. Asali ina uwezo mdogo sana wa kuyeyuka katika maji, kwa hiyo iwapo maji yatachafuka ujue kwamba asali hiyo imechakachuliwa.
2. Mwaga asali chini kwenye mchanga.
Katika jaribio hili iwapo mchanga utalowana, ujue asali hilo imefanyiwa maujanja. Asali halisi 100% haiwezi kulowanisha mchanga.
3. Weka asali kwenye karatasi nyeupe.
Katika jaribio hili, iwapo asali itakua imechakachuliwa kwa kuongeza maji au sukari italowanisha karatasi kwa haraka. Asali halisia 100% haiwezi lowanisha karatasi kwa haraka, itachukua mda mrefu kulowanisha karatasi.
4. Weka asali kwenye kijiko na uimwage taratibu
Kwa jaribio hili utaweza kuijua asali ambayo haijachakachuliwa itamwagika bila kukatika, wazungu wanasema " Ze honey will form a single line". Ukiona asali yako inakatika na kufanya kama matone hivi ujue umeuziwa asali iliyowekwa maji.
5. Kuchovya asali kwenye kitambaa cha pamba na kukiwasha kwa njiti kiberiti.
Iwapo kitambaa kitawaka asali hiyo haijachakachuliwa. Kama imewekewa maji kitambaa hakitawaka.
  • Hitimisho.

Kuna njia nyingi za kimaabara ambazo zinaweza kufanyika kujua kama imechakachuliwa, njia hizo tano nilizo kuelekeza ni hatua za awali na za mwanzo kabisa unao weza kuzifanya kabla haujashikishwa asali feki.


1 comment :