Wednesday, July 15, 2015

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA YAPO HAPA

Matokeo ya kidato cha sita yametoka.
Kupata matokeo hayo bofya HAPA

HASARA YA KULIFANYIA MTAJI WA BIASHARA JINA LA LOWASA


Kama ilivyojadi kwa wajasiriamali na 
wachakarikaji ya kutumia "opportunity" zinazojitokeza kufanya biashara, hiyo ni moja ya picha nilizozipata huko WhatsApp na kwenye 'social media', inawezekana kabisa kuwa biashara nyingi zilipangwa kwa kutumia jina la Lowasa kama mtaji kwa imani kuwa angekuwa Rais wa Tanzania mwaka huu.

MGOMBEA URAISI UKAWA BADO NGOMA NZITO

Waandishi wa habari wakisubiri kwa hamu Tamko la Viongozi wa UKAWA
Waandishi wa Habari kutoka vyomba mbalimbali vya habari walipiga kambi siku ya jana katika Hoteli ya Colosseum iliyopo Masaki kutokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa jana ndiyo ilikua siku rasmi ya kutangaza jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA.

DK. MAGUFULI ANG'ARA VIWANJA VYA ZAKHIEM MBAGALA

Mgombea mteule wa urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, Dk John Magufuli ametambulishwa rasmi leo katika viwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika viwanja hivyo, Magufuli alisema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha haki inatendeka kwa Watanzania wote.

MFANYA BIASHARA MAARUFU JIJINI MWANZA AFANYA MAUAJI YA KUTISHA


Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara maarufu Jijini humo Juma Mahende, anayemiliki Mabasi ya J4 kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili na kuwapotezea maisha, katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato Jijini humo.