Akizungumza katika viwanja hivyo, Magufuli alisema iwapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha haki inatendeka kwa Watanzania wote.
“Nataka niseme kwa dhati sitawaangusha, nitafanya kazi kweli kweli, sitamuogopa mtu na wala sitapenda mtu wa chini aonewe,” alisema Dk Magufuli.Aliongeza kuwa atahakikisha anasimamia Ilani ya CCM na kuitekeleza. Magufuli aliwashukuru Watanzania kwa sala zao kwani katika mchakato mzima alikuwa akiwasihi wamuombee. “Kupitishwa kwangu inadhihirisha wazi mlikuwa mnaniombea na sala zenu zimesikilizwa na mwenyezi Mungu ” alisema.
No comments :
Post a Comment