Waandishi wa habari wakisubiri kwa hamu Tamko la Viongozi wa UKAWA |
Waandishi wa Habari kutoka vyomba mbalimbali vya habari walipiga kambi siku ya jana katika Hoteli ya Colosseum iliyopo Masaki kutokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa jana ndiyo ilikua siku rasmi ya kutangaza jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA.
Tukio hilo halikuweza kufanyika kutokana na kikao hicho kuendelea kwa muda mrefu bila ya jina hilo kutangazwa.
Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari juu ya kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, alisema majadiliano yao siyo ya urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kamera za waandishi wa habari |
Makene amewataka waandishi wa habari wawe na subira kwa ajili ya maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo.
Hata hivyo baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana, waandishi wa habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA wakajikuta wanaacha stendi za kamera zao na kukaa pembeni kama zionekanavyo pichani usiku huu, wakisubiri lolote litakalojiri.
Mpaka kufika majira ya saa mbili usiku bado mgombea wa Uraisi bado alikua hajatangazwa
No comments :
Post a Comment