wachakarikaji ya kutumia "opportunity" zinazojitokeza kufanya biashara, hiyo ni moja ya picha nilizozipata huko WhatsApp na kwenye 'social media', inawezekana kabisa kuwa biashara nyingi zilipangwa kwa kutumia jina la Lowasa kama mtaji kwa imani kuwa angekuwa Rais wa Tanzania mwaka huu.
Hata hivyo walisema wahenga kuwa huwezi kufanikiwa usipojaribu na katika biashara kuna kupata na kukosa. Hivyo, pamoja na hasara, isiwe ndiyo mwisho wa kujaribu baada ya kujifunza.
Ni vyema kuifanyia biashara siasa katika ujumla wake. Badala ya kujikita kwenye kufanya biashara ya mgombea fulani, ni afadhali kuwekeza kwenye chama kwa sababu wataendelea kubakia wanachama katika chama hicho licha ya kuwepo tofauti za wagombea au hata wanachama wake.
Njia ya mkato ya kutafuta kujipatia kipato kikubwa kwa haraka katika muda mfupi ni sawa na kucheza kamari kwa imani kuwa mzunguko unaokuja ndiyo nafasi yako ya kuvuna mamilioni, ukasahau kuwa mnaotarajia hivyo mpo wengi zaidi ya nafasi
No comments :
Post a Comment